Comments


FULU VIDEO>.AFANDE SELE NIKIFA MWILI WANGU UCHOMWE MOTO





















‘Hii ni imani ambayo nimeifikiria muda mrefu na nikajua lazima niifate, kila mtu ana kitu ambacho anakiamini na kwangu naamini moto ndio kila kitu kwenye maisha, kama maandiko yanavyosema Mungu ni moto ulao… naamini moto ndio mfumo ambao hata Mungu anatokana na moto wenyewe‘ – Afande Sele Kwenye sentensi ya pili Afande amesema ‘wakisema Mungu hajulikani au Mungu hujui ni kitu gani hapo kwangu siwezi kuamini kitu ambacho hakionekani kwa hiyo mimi naamini Mungu ni lile jua linalowaka sababu ndio moto mkuu kuliko mioto yote, sasa kama Mungu ni moto ulao basi mimi napaswa niliwe na moto ule‘ ‘Naamini nikichomwa moto nitakua majivu, unaposema Mungu ni moto ulao inamaana mimi moja kwa moja nitakua nimeliwa nimeingia ndani ya Mungu mwenyewe, hata kesho nikifariki nikachomwa moto nikawa majivu, sipendi kufufuliwa kwenye mazingira ya ubinaadamu tena sababu nimegundua ubinaadamu sio kitu kizuri cha kujivunia‘ ‘Japo binadamu wanaweza kujivunia sababu ndio wanatengeneza Ndege, Magari na vitu vingine…. binadamu ndio kiume mbaya na muovu, msaliti, mnafiki, batili kuliko kiumbe chochote katika ulimwengu, hata dunia yenyewe itamalizwa na binadamu na sio kiumbe mwingine kwahiyo ili kuukana huu ubinadamu sipaswi kuzikwa kwenye udongo, nikizikwa kwenye udongo manake nitafufuliwa kama binadamu tena kitu ambacho sikitaki‘ – Hayo ni maneno ya Afande Sele msanii wa siku nyingi kwenye muziki wa bongofleva Kwa kumalizia, Afande amesema ‘Mungu ninaemwamini mimi ni moto na moto mkuu kuliko yote ni jua hata samaki anayeishi chini ya bahari kabisa jua likiwaka asubuhi anatoa mgongo juu inamaana anatoa heshima yake kwa Mungu, hiyo ndio imani yangu na wala simlazimishi mtu mwingine yeyote aamini ninavyoamini mimi, hata familia yangu na watoto wanajua baba akifa anatakiwa kuchomwa moto
KAULI YAKE KWA NYIA YA VIDEO HII HAPA TAZAMA
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system