AL AHLY YATUA DAR KWAAJILI YA KUMENYANA NA YANGA
Uongozi wa klabu ya Dar Es Salaam Young Africans leo April 6 kupitia kwa afisa habari wake
Jerry Muro ameongea na vyombo vya habari na kuelezea taarifa za mchezo wao wa klabu
Bingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaochezwa April 9 2016 uwanja wa Taifa Dar
Es Salaam.
Jerry amethibitisha Al Ahly kuwasili Dar Es Salaam alfajiri ya leo, pamoja na CAF kutoa majina
ya waamuzi wa mchezo huo ambao wanatoka Ivory Coast Denis Dembele, Mauris Donatien,
Moussa Bayere, Tangba Kambou lakini kamisaa wa mchezo Celestine Ntangungira anatokea
Rwanda.
Hadi sasa Yanga mechi zao zilizopita za klabu Bingwa Afrika waligoma zisioneshwe kwenye TV ”
Kwa sasa viongozi wanafanya utaratibu wa kuangalia namna ambavyo tunaweza kuruhusu TV
kuonesha mchezo huo, lakini watu wajue tutaruhusu matangazo ya TV yarushwe mikoani kasoro
Dar na Pwani ndio maana tumeweka kiingilio cha chini elfu tano” >>> Jerry Muro
0 comments:
Post a Comment