Comments


SIMBA ALALA MBELE YA TOTO AFRICANS

Simba imejiweka katika mazingira magumu ya kuwa mabingwa wa Ligi ya Vodacom Tanzania baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0, kutoka kwa Toto Africans ikiwa nyumbani
Timu ya Simba leo imejiweka katika mazingira magumu ya kuwa mabingwa wa Ligi ya Vodacom Tanzania baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0, kutoka kwa Toto Africans ikiwa nyumbani uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Kipigo hicho kinawafanya Simba kubakia nafasi ya pili wakiwa na pointi 57, huku wakicheza mechi 25, na kuzizidi klabu za Yanga inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 59 na michezo 24 sawa na Azam FC, lakini yenyewe ikiwa nafasi ya tatu wakiwa na pointi 55.
Licha ya kipigo hicho lakini Simba walilazimika kucheza bila ya maelekezo ya kocha wao Jackson Mayanja kuanzia dakika ya 33, baada ya kupinga maamuzi ya mwamuzi Ahamada Simba lakini pia kipindi cha pili ilimpoteza beki wake wa kulia Hassan Ramadhani Kessy kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 47 kwa kumchezea rafu mbaya Edward Cristopha.
Hadi mapumziko Toto Africans walikuwa mbele kwa bao la mapema lililofungwa dakika ya 20 na mshambuliaji Wazir Junior, alipiga shuti kali baada ya kupokea pasi ya kichwa kutoka kwa Cristophar.
Bao hilo lilitokana na shambulizi la kustukiza lililofanywa na Toto, baada ya vijana hao kuokoa mpira wa kona iliyopigwa kwenye lango lao.
Kuingia kwa bao hilo kuliinzidua Simba ambayo leo mashambulizi yake yaliongozwa na Hamisi Kiiza na Danny Langa ambao walionekana kukosa maelewano na kumuacha kipa wa Toto Afrika Mussa Kirungi akifanya atakavyo.
Simba iliendelea kufanya mashambulizi mengi kwenye lango la Toto hasa baada ya kumuingiza mshabuliaji wake Ibrahim Ajibu lakini waliendelea kupoteza nafasi nyingi za mabao.
Kinara wa mabao wa Simba Hamisi Kiiza, alionekana kutokuwa mchezoni kutokana na kubanwa vilivyo na mabeki w Toto.
Baada ya mchezo huo kumalizika mashabiki wa timu hiyo walimvamia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe, na kuhoji kwanini timu yao imepoteza huku wakimmwagia mchanga ambaye naye aliingia kwenye gari yake na kutoa Bastola na kuondoa gari yake kwa kasi na kuwachangua watu wote waliokuwa wamemzunguka.
Baada ya tukio hilo Polisi waliingilia kati na kupiga mabomu kwa ajili ya kuwatawanya mashabiki hao na kiongozi huyo kuondoka zake uwanjani hapo akiwa salama.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system