Comments


WIZARA YA ELIMU AKANUSHA WALIMU KUANDALIWA SARE.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako.

Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imekanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii kuwa Waziri wake Profesa Joyce Ndalichako ametaka walimu kuandaliwa sare.


Taarifa iliyotolewa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini inasema kuwa taarifa hizo si za kweli na kuwaonya watu wanaotoa taarifa za uzushi kuacha mara moja. Imesema imejipanga kuhakikisha inachukua hatua za kisheria kwa watakaobainika kuanzisha na kueneza uzushi huu.

“Tunapenda kuufahamisha umma kuwa taarifa hizi si za kweli. Watu wanaoeneza taarifa za kizushi za aina hii waache kufanya hivyo ili kuepusha usumbufu unaojitokeza,” ilisema taarifa hiyo.

 Taarifa zilizokuwa zimeenea kwenye mitandao zinasema kuwa Profesa Ndalichako amesema nguo kwa ajili ya walimu zinaandaliwa ambazo zitakuwa aina tatu.

Sare hizo zitakuwa ni mashati matatu meupe yenye nembo ya taifa, suruali na sketi zitakuwa za rangi ya bluu, kijani na kaki na kofia yenye nembo ya taifa.

 Ilidai mwongozo wa uvaaji sare hizo utatolewa na kusisitiza kuwa kila mwalimu atatakiwa kwenda kazini akiwa na sare ambayo ataivaa hadi muda wa kazi utakapoisha ambao utakuwa ni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi 12:00 jioni.

Taarifa hiyo inayonukuu chanzo cha habari cha gazeti moja la Kiswahili (sio HabariLeo) zilidai kazi hiyo ya kuandaa sare hiyo itakamilika Mei Mosi mwaka huu na wakuu wa shule kutakiwa kwenda kuchukua sare hizo katika ofisi za halmashauri
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system