Chama cha soka nchini Uingereza FA kimebainisha kuwa Jamie Vardy atakosa mchezo muhimu wa klabu ya Leicester dhidi ya Manchester United jumapili ijayo kwa adhabu ya nyongeza ya mechi kutokana na utovu wa nidhamu.vardyChama cha soka nchini Uingereza FA kimebainisha kuwa Jamie Vardy atakosa mchezo muhimu wa klabu ya Leicester dhidi ya Manchester United jumapili ijayo kwa adhabu ya nyongeza ya mechi kutokana na utovu wa nidhamu.
Leicester itahitaji kushinda mchezo huo ili kunyakua ubingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza lakini kumkosa Vardy huenda ikawa na wakati mgumu.
Mpinzani wa Leicester katika mbio za ubingwa, klabu ya Tottenham imewapa nafasi mbwea hao, baada ya kutoka sare ya 1-1 na Westbrom, na hesabu za ubingwa ni kushinda mechi moja kati ya 3 zilizobaki.
Vardy aliyekuwa mwiba kwa mabeki kwenye msimu huu, alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuzozana na mwamuzi wa mchezo ulioisha kwa sare ya 2-2 dhid ya Westham April 17 mwaka huu.
FA pia imeipiga faini paundi, 20,000 klabu ya Leicester kwa kushindwa kudhibiti wachezaji wake kwa kuonyesha utovu wa nidhamu.
0 comments:
Post a Comment