Wabunge
wa Upinzani wamesema wao walikuwa hawasaini posho kama naibu spika
anavyodai na wanataka posho hizo kufutwa kabisa kama serikali ya JPM
inataka kubana matumizi kweli
Mheshimiwa
Spika, kabla sijatoa maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani kuhusu bajeti ya
Serikali ya 2016/17, napenda kuweka rekodi sawa kuhusu upotoshaji
unaofanywa na Wabunge wa CCM kwamba Wabunge wa Upinzani wanaisaini
mahudhurio bungeni na kuchukua posho bila kufanya kazi.
Napenda
mkumbuke kwamba, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imekuwa ikisisitiza
kufutwa kwa posho za vikao kwa maana ya “Sitting allowance”, lakini
serikali imekuwa ikipata kigugumizi, hivyo basi Kambi Rasmi inasema kama
kweli Serikali ya Rais John Pombe Magufuli inania thabiti ya kubana
matumizi ya Serikali basi inoneshe uthabiti huo kwa kuifuta posho ya
vikao na fedha hizo zipelekwe kwenye miradi ya maendeleo hususani
kuwapatia Watanzania maji safi na salama.
Hata
hivyo, tunashauri, wale wanaokaa bungeni bila kuchangia hata kwa
maandishi na kuchukua posho, wafuatiliwe na wakatwe mishahara yao, kwa
kuwa hawajafanya kazi na hansard itumike
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment