Comments


POLISI KUJENGEWA NYUMBA 4139KATIKA MIKOA 17 NCHINI.

SERIKALI
katika
mwaka
2016/17
imepanga
kujenga
nyumba 4139 za askari wa jeshi la Polisi nchini,
hatua itakayosaidia kukabiliana na uchache wa
nyumba za kuishi kwa askari hao.
Awamu ya kwanza ya nyumba hizo zinatarajiwa
kujengwa katika mikoa 17 nchini ikihusisha
mikoa ya Tanzania Bara pamoja na mikoa ya
Unguja na Pemba.
Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM),
Faida Mohammed Bakar, Naibu Waziri wa
Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha
alisema Serikali itaendelea kuboresha makazi ya
askari na ofisi za polisi kwa awamu kwa kadri
hali ya kiuchumi itavyoimarika.
Ole Nasha alisema Serikali inatambua
changamoto zinazowakabili askari polisi katika
maeneo mbaliombali nchini ikiwemo uchakavu
wa ofisi, ambapo kwa kuanzia imeamua kuanza
mpango wa kukarabati ofisi na makazi ya askari
wake.
Aidha alisema Serikali pia imekusudia
kuhakikisha kuwa inatoa mikopo ya vyombo vya
usafiri kwa askari wake ambao wanaishi mbali
na vituo vyao vya kazi ili kuwasaidia kuwahi
katika maeneo yao ya kazi kwa wakati.
“Serikali inatambua changamoto inayowakabili
askari wetu nchini ikiwemo wale wa Kusini
Pemba, katika kukabiliana na hali hiyo
tumepanga sasa kuifanyaia ukarabati
miundombinu ya ofisi hiyo sambamba na ujenzi
wa makazi bora kwa askari wetu” alisema Ole
Nasha.
Katika swali lake, mbunge huyo alitaka
kufahamu mikakati ya Serikali ya kujenga
nyumba za kuishi Na ofisi za kisasa katika kituo
cha mkoani na kengeja Pemba.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system