Comments


MEXICO YAICHAPA URUGUAY 3-1.

Mashindano ya kusaka Nchi Bingwa wa Copa América Centenario yameendelea kwa Mechi za Kundi C na D huko Nchini USA.

Kwenye Kundi C Venezuela iliichapa Jamaica 1-0 kwa Bao la Dakika ya 16 la Josef Martinez na Mechi nyingine ya Kundi hilo, Mexico iliitwanga Uruguay 3-1 kwenye Mechi ambayo kila Timu ilimaliza Mtu 10.

Bao za Mexico zilifungwa na Alvaro Pereira, aliejifunga mwenyewe Dakika 4, Rafael Marquez, 85, Hector Herrera, 92 na Uruguay kupata Bao lao Dakika ya 74 kupitia Diego Godin.

Uruguay walibaki Mtu 10 kuanzia Dakika ya 45 baada ya Matias Vecino kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu na Mexico nao kubaki 10 kuanzia Dakika ya 73 baada ya Andres Guardado kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa kwa Kadi Nyekundu.


Mashindano haya Copa América Centenario ni mahsusi kusheherekea Miaka 100 ya Copa America, Mashindano ya Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kusini, CONMEBOL, ambayo yalianzishwa Mwaka 1916.

Hii ni mara ya kwanza kwa michuano hii kuchezwa nje ya Marekani ya Kusini.

Haya yatakuwa ni Mashindano ya 45 kufanyika na kawaida yake hufanyika kila baada ya Miaka Minne lakini safari hii CONMEBOL na CONCACAF, Shirikisho la Soka la Nchi za Marekani ya Kaskazini, Kati na Nchi za Visiwa vya Caribbean, walikubaliana kuandaa Mashindano maalum.

Safari hii michuano hii itakuwa na Nchi 16, badala ya 12 za kawaida, kwa kushirikisha Nchi 10 kutoka CONMEBOL na 6 za CONCACAF.

Kawaida Mshindi wa Copa America huiwakilisha Marekani ya Kusini kwenye Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho lakini Mshindi wa Copa América Centenario hatapewa hilo kwani Mwaka Jana Chile, wakiwa Nyumbani kwao, ndio walitwaa Copa America ya kawaida na wao ndio watashiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Shirikisho Mwakani, 2017, huko Russia.


Kwenye Mechi nyingine zilichochezwa Usiku wa Jana, Costa Rica na Paraguay za Kundi A zilitoka 0-0 na kwenye Kundi B Peru iliifunga Haiti 1-0 kwa Bao la Dakika ya 61 la Paulo Guerrero.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system