Timu ya taifa ya Brazil imekumbana na wakati
mgumu katika mchezo wa Copa America 2016
dhidi ya Peru uliochezwa alfajiri ya June 13
2016, mchezo huo wa Kundi B ulikuwa unawapa
nafasi kubwa Brazil kuibuka na ushindi, hususani
takwimu ya kumiliki mpira kwa asilimia 66 ili
wafanya Peru wacheze kwa kulinda goli zaidi.
Licha ya kuwa Brazil kuwa nafasi ya 7 katika
viwango vya FIFA na Peru nafasi ya 48,
walikubali kuruhusu goli dakika ya 75 baada ya
Raul Ruidiaz kufanikiwa kufunga goli
linaloaminika kuwa la mkono kwa wachezaji wa
Brazil , goli hilo lilifanya mchezo kusimama na
muamuzi kuvuta muda wa kufanya maamuzi.
Ujanja wa Raul Ruidiaz umeisaidia Peru kutinga
hatua inayofuata na kuifanya Brazil kufungasha
virago na kurejea Brazil , baada ya mchezo huo
Brazil wamesalia na point 4 wakiwa nafasi ya
tatu nyuma ya Ecuador na Peru anayeongoza
kwa jumla ya point saba.
0 comments:
Post a Comment