MAKOCHA wanane kutoka nchi nane
tofauti wamejitosa kuifundisha timu ya
Simba ya Dar es Salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Simba,
Geofrey Nyange ‘Kaburu’, alisema jana
kuwa kitu cha kwanza wanachokusudia
kukifanya ni kuleta kocha Mzungu
mwenye rekodi ya kimataifa, ambaye
atawasaidia kuwaongoza kuchagua
wachezaji wa kusajili ili kuwa na kikosi
imara.
“Bado tunaendelea na mchakato wa
kusaka kocha, tayari tuna maombi kutoka
kwa makocho wa nchi nane tofauti. “Wapo
wawili ambao tumevutiwa nao na
tunatarajia kufanya nao mazungumzo ili
kuona yupi tumchukue,” alisema Kaburu.
Alisema hawawezi kutaja nchi
wanazotokea makocha hao, lakini
kilichowavutia ni ubora wa wasifu wao na
kulifahamu vizuri soka la Afrika hasa
ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
Alisema mbali ya kuwahi kufanya kazi
kwa muda mrefu Afrika, lakini pia
wanayajua vizuri mazingira ya kazi na
maisha ya wachezaji wenyewe, hivyo
itakuwa rahisi kwao kuijenga timu yao na
kupata mafanikio kwa muda mfupi.
“Shida yetu kubwa ni kuiona Simba
ikifanya vizuri kwenye ligi na kumaliza
uteja wa kufungwa na Yanga kama
ilivyokuwa msimu uliopita, ndiyo maana
tukaamua kutafuta kocha mwenye kulijua
vizuri soka la Afrika Mashariki na
wachezaji wenyewe na tunafurahi
mazungumzo yanaenda vizuri,” alisema
Kaburu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment