Waziri wa nchi na Ofisi ya makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe.January
Makamba amesema kuwa wameandaa
mashindano ya upandaji wa miti na
ufufuaji visiki hai katika ngazi zote nchini
ili kufanikisha mapinduzi ya kijani na
kutoa kiasi cha pesa cha shilingi milioni
100 kwa halmshauri itakayofanya vizuri.
Waziri makamba ameyasema hayo
alipokuwa akifunga warsha ya siku moja
kwa wabunge kuhusu kukabiliana na tishio
la jangwa na kuboresha ardhi iliyochakaa
ili izalishe zaidi katika ukumbi wa Bunge
wa Pius Msekwa jijini Dodoma.
Aidha amesema kuwa atashirikiana na
Tamisemi na Wizara ya elimu kuhakikisha
elimu ya upandaji miti na ufufuaji wa
visiki hai inatolewa kuanzia ngazi ya elimu
ya Awali ili wanafunzi waanze kupata
elimu hii kuanzia katika ngazi ya chini.
Mhe.Mkamba alisema kuwa upandaji wa
miti ndio utaleta manufaa makubwa nchini
mwetu kwani hakuna sekta isiyotegemea
miti toka uumbwaji wa dunia hii kwani
Nyanja za Afya,ufugaji,misitu,utalii na
maji zote zinategemea uhifadhi wa
Mazingira yetu.
Aidha waziri huyo mwenye dhamana ya
mazingira alisema kuwa kama jamii yetu
haitahifadhi mazingira basi hakuna sekta
itakayofaidika na kuongeza kwamba
atasimama kidete kutengeneza mikakati
ya maendeleo juu ya mazingira.Pia
amehaidi Serikali kutenga fedha za
kutosha,kutengeneza Sera nzuri,sheria na
miongozo yenye tija katika mipango ya
maendeleo.
Katika upande mwingine amesema kuwa
kwa sasa utaratibu wa kufufua visiki hai ni
jambo ambalo litawekwa katika mpango
wa maendeleo ya Taifa na kuzitaka wizara
zinazohusiana na mazingira kushirikisha
watu wote ikiwemo kuwapa elimu kuhusu
ufufuaji wa visiki hai.
Aidha Waziri Makamba amesema kuwa
serikali ina mkakati mkubwa wa
uboreshaji wa Sera za Mazingira uku
mkakati wa kupanda na kutunza miti wa
mwaka 2016-2021 ukiwa bado katika
mipango mahususi ya kuifanya Tanzania
kuwa ya Kijani.
Warsha hiyo kwa wabunge imeeandaliwa
na shirika la Lead foundation uku
ikishirikisha ofisi ya Bunge na wadau
kutoka World Vision, Ever Green na World
Agroforestry Center ambao walitoa mada
mbalimbali kwa wabunge ikiwemo jinsi ya
kuhifadhi Uoto wa Asili, Kilimo cha
kijani,namna ambavyo ufufuaji wa Visika
hai na Ngitili zinavyoweza kuchangia
Mpango wa kitaifa wa Upandaji Miti na
kuimarisha mshikamano kitaifa wa
ustawishaji Miti.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment