Comments


picha pamoja na video jinsi ureno walivyofanikiwa kumfungasha virago poland











Mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Uefa Euro 2016 umepigwa katika dimba la Stade Velodrome nchini Ufaransa , mchezo ulitizamwa na mashabiki 62,000 na kushuhudia Ureno ikifuzu kucheza hatua ya nusu fainali mbele ya Poland.
Awali mchezo huo ulimalizika kwa sare ya goli 1-1 na kuongezwa dakika 30 ambazo nazo zilishindwa kutoa mshindi wa mchezo nddipo mwamuzi Felix Brych kutoka Ujerumani akaamua ipigwe katika mikwaju ya penati ambapo Ureno ilifanikiwa kupata ushindi wa penati 5-3.
Kwa matokeo hayo Ureno imepata nafasi ya kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali mchezo utakaochezwa Juni, 6 na atapambana na kati ya Ubelgiji au Wales.
Lakini pamoja na hatua ambayo mpaka sasa Ureno wamefikia na kucheza michezo minne, wameibuka na ushindi katika dakika 90 kwa mchezo mmoja pekee dhidi ya Croatia, mingine iliyosalia imekuwa ikitoa sare ikiwepo ile ya hatua ya makundi ambapo ilimaliza na alama tatu kwa kutoa sare michezo yote.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system