Comments


UTARATIBU WA CHAKULA ,MUHIMBILI WASIMAMISHWA KWA MUDA.

Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, ameagiza utaratibu mpya wa Hospitali ya Muhimbili kutoa chakula kwa wagonjwa usimame kwanza ili kupata taarifa kuhusu faida na hasara zake.

Wananchi mbali mbali walitao maoni yao juu ya utaratibu huo mpya ambao ulitakiwa kuanza kufanya kazi kuanzia tarehe 1 mwezi wa saba, wapo watu ambao walikuwa wanaunga mkono lakini kundi kubwa la watu walikuwa wakipinga suala hili wakisema kuwa Hospitali haitaweza kutoa huduma bora kwa wagonjwa hususani kwenye chakula.ummy-Mwalimu29Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hata wao wamesikia maoni na ushauri wa wananchi juu ya utaratibu huo mpya na kuamua kusimamisha zoezi hili ili wajipange kwanza.

“Wizara masikio tumesikia maoni na ushauri kutoka kwa wananchi, wengine wanaona utaratibu mzuri wengine wanaona ni mbaya. Lakini kubwa tunazidi kusisitiza kuwa Hospitali ya Taifa ipo wakati itabidi ibaki kama Hospitali ya Taifa, hata hii hudumu ilipendekezwa kwa ajili ya kuboresha huduma ila jambo hili limekuja kwa haraka sana, kwa hiyo nimeagiza Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kusimamisha utaratibu huo mpya wa kutoa chakula kwa wagonjwa hadi pale ambapo tutakuwa na taarifa za kutosha kuhusu harasa na faida za utaratibu mpya unaopendekezwa, kwa hiyo nimeshatoa maelekezo hautaanza tujipange kwanza kwa mwezi mmoja au miwili” alisema Waziri Ummy Mwalim
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system