Comments


GWAJIMA KUSAKWA NA POLISI

Baada ya kuweka kambi kwa zaidi ya saa saba
nyumbani kwa Askofu Josephat Gwajima wa
kanisa la Ufufuo na Uzima, Jeshi la Polisi
limesema bado linamsaka kiongozi huyo wa
kiroho usiku na mchana.
Juzi askari wa jeshi hilo, Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam walishinda mbele ya geti la
nyumba ya askofu huyo kwa zaidi ya muda huo
bila kufunguliwa na kuondoka bila kumkamata,
hiyo ikiwa ni mara ya pili kwa chombo hicho
cha dola kufanya hivyo katika kipindi cha miezi
16.
Baada ya kushindwa kumtia nguvuni mapema
mwaka jana, Askofu Gwajima alijisalimisha
kituoni siku iliyofuata.
Lakini jana, Gwajima hakufanya hivyo, na
haijulikani alipo. Kamanda wa Kanda ya Dar es
Salaam, Simon Sirro amesema wanaendelea
kumtafuta askofu huyo na kuwataka wenye
taarifa za mahali aliko, waisaidie polisi.
Akieleza sababu za kwenda nyumbani kwake
bila ya kumtaarifu askofu huyo, Kamanda Sirro
alisema hawalazimiki.
“Si lazima apelekewe taarifa, askari walikwenda
kwa nia njema ya kuonana naye ndiyo maana
hawakutoa taarifa,” alisema Sirro na kuongeza:
“Kama amejificha, tukimbaini alipo tutamkamata
na atambue bado tunamtafuta.”
Askofu Gwajima anatafutwa na polisi katika
kipindi ambacho mkanda unaodhaniwa una sauti
yake, umezagaa kwenye mitandao ya jamii.
Sauti kwenye mkanda huo inasema Rais wa
Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete
afikishwe mahakamani kwa yote yaliyofanyika
wakati wa utawala wake ambayo rais wa sasa,
John Magufuli anayashughulikia.
Pia, sauti hiyo inadai kuwa baadhi ya viongozi
wa CCM wametuma watu mikoani kupiga
kampeni ya kutaka Magufuli asipewe uongozi
wa chama hicho kwa sasa kama ilivyo utaratibu
wa chama hicho.
Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina
yao kwa kile walichodai si wasemaji wa familia
wala kanisa, watu wa karibu na askofu huyo
walisema wanashangaa kuona polisi
wanamtafuta bila kufuata taratibu kama
kumuandikia barua.
Mmoja wa watu hao alisema hadi sasa
wanashindwa kufahamu kama waliokuja kwa
askofu ni askari kama inavyoelezwa au
majambazi kwa sababu hawakuwa na sare wala
vitambulisho.
Alisema sababu anayotafutiwa Gwajima ni
kukinanga chama, wanaomtafuta ni wana
usalama ambao hawatakiwi kuwa na chama
kitu ambacho kinatia shaka.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system