Comments


YANGA YATUMIA MILIONI 240 KUMNASA MSHAMBULIAJE WA ZAMBIA

YANGA imemnasa mshambuliaji mpya
raia wa Zambia, Obrey Chirwa
anayechezea klabu ya Platinum FC ya
Zimbabwe kwa kitita cha dola za
Marekani 120,000 (zaidi ya Sh milioni 240
za Tanzania).
Kwa mujibu wa gazeti la The Herald la
Zimbabwe jana lilieleza kuwa Chirwa
ambaye amewahi kuichezea timu ya
Konkola Blades ya Zambia, ameifungia
Platinum mabao matano katika mechi
nane alizocheza kwenye Ligi Kuu ya
Zimbabwe.
Chirwa, ambaye yumo kwenye kikosi cha
timu ya taifa ya vijana ya Zambia chini ya
umri wa miaka 23 imeelezwa na gazeti
hilo kuwa aliondoka Zimbabwe juzi kuja
Dar es Salaam na alitarajiwa kuwasili Dar
es Salaam jana.
Chirwa anatarajia kushirikiana na
mshambuliaji mahiri wa Yanga Donald
Ngoma, ambaye pia ametokea timu hiyo
ya Zimbabwe. Awali Yanga ilikuwa
ikimuwania winga Walter Musona kutoka
Platinum kabla ya kughairi dakika za
mwisho na Chirwa kuonekana mtu sahihi
kwa nafasi hiyo.
Viongozi wa Yanga hawakupatikana jana
kuzungumzia suala hilo na hata Kocha
Mkuu wa timu hiyo, Hans Pluijm ambaye
yupo Algeria na Yanga, alipotafutwa kwa
njia ya mtandao kuhusu usajili huo
alisema hana cha kuzungumza.
Wakati huohuo, Yanga iliwasili salama
jana asubuhi nchini Algeria tayari kwa
mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho
la Soka Afrika (CAF CC) dhidi ya wenyeji
MO Bejaia. Nahodha wa timu hiyo Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ alisema wachezaji
wote wapo katika ari ya ushindi kwa ajili
ya mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa
Unite Maghrebine mjini Bejaia, Algeria.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system