MAHAKAMA ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara
imemhukumu, Ally Mpemba au Ustadhi (32),
Mkazi wa Mtaa wa Bunda Stoo mjini Bunda
kifungo cha miaka 60 jela baada ya kupatikana
na hatia ya kubaka watoto wawili kwa zamu
akijifanya polisi.
Adhabu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu wa
Mahakama ya wilaya ya Bunda, Said Kasonso,
baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo pasipo kuacha shaka yoyote.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo na Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, Hamuza Mdogwa, kuwa
mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo
Januari 17 mwaka huu, majira ya saa 8:30
mchana, katika kijiji cha Kitaramanka wilayani
hapa.
Alisema kuwa mshtakiwa huyo aliwakuta watoto
hao wakiwa katika eneo hilo na akawatisha
kuwakamata akidai kuwa yeye ni askari Polisi
na kwamba wamefanya kosa hivyo atawachukua
maelezo yao na baadaye awapeleke kituoni.
Aliongeza kuwa mshtakiwa huyo alitoa Sh 200
na kumpatia mtoto mmoja aende akanunue
daftari la kuandikia maelezo yao, na baada ya
mtoto huyo kwenda ndipo alipombaka aliyebaki
na kisha kumwambia adhabu yake imekwisha
sasa aende nyumbani.
Alisema kuwa baada ya yule aliyetumwa daftari
kurudi, Mpemba alimbaka pia na kumuamuru
arudi nyumbani adhabu yake imekwisha na
kwamba watoto hao baada ya kufanyiwa
unyama huo walikwenda kutoa taarifa nyumbani
kwa wazazi wao.
Aidha alisema kuwa Ofisa Mtendaji wa kata
hiyo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji
hicho walimkamata mshtakiwa huyo na
kumfikisha Polisi.
Kabla ya adhabu kutolewa mshtakiwa huyo
alipewa fursa ya kujitetea na akaiomba
Mahakama hiyo impunguzie adhabu.
Hata hivyo mwendesha mashitaka huyo
aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa
mshtakiwa huyo kwa sababu makosa aliyofanya
ni ya kinyama na ya udhalilishaji mkubwa kwa
watoto hao wenye umri wa miaka 16 kila
mmoja.
Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Kasonso, alisema
kuwa ameridhika na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo na kwamba kwa kosa la
kwanza la kubaka mtoto wa kwanza ataenda
jela miaka miaka 30 na la pili pia atatumikia
kifungo cha miaka 30 jela na adhabu zote
zinakwenda kwa pamoja hivyo atatumikia
kifungo cha miaka 30 jela ili iwe fundisho kwake
na kwa watu wengine wenye nia na tabia kama
hiyo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment