Baadhi ya watu wamekuwa wanachukulia
kirahisi ulaji wa matunda, lakini unapaswa kujua
kwamba matunda ni muhimu kwa afya zetu
kwani yanatukinga na magonjwa mbali mbali na
pia hutengeneza muonekano mzuri wa ngozi ya
miili yetu.
Kunakila sababu za kukubali kuwa matunda ni
muhimu sana kwa afya zetu kwa sababu
huongeza vitamin kibao; zifuatazo ni sababu
zinazokufanya ule matunda kila siku:
AVOCADO : Tunda hili limekuwa maarufu sana
kwa kutengenezewa juice, lakini huenda watu
wakawa hawalipendi kwasababu ya kutokuwa na
sukari katika radha yake. Tunda hili linavitamini
kibao, ambapo pia huongeza mafuta mwilini, kwa
wale walitumialo mara kwa mara.Unashauriwa
kula au kunywa juice ya avocado wakati wowote
endapo kama huna matatizo yoyote
yanayohusiana na kuzidi kwa mafuta mwilini.Pia
tunda hili huongeza uzito endapo utalitumia
mara kwa mara.
APPLE: Hili ni tunda maarufu sana duniani
lihusishwalo na wapendanao, lakini tunda hili
pamoja na kupewa umaarufu mkubwa duniani na
kuwa na vitamini na madini kibao, pia lina kazi
kubwa sana katika kukupa muonekano mzuri wa
ngozi ya mwili wako.Tunda hili husaidia
kuboresha mzunguko wa damu mwilini pamoja
na kuhifadhi ngozi isipoteze uhalisia wake.
NDIZI: Hili pia ni tunda lenyejina kubwa kwa
watu wengi wanaojali ulaji wa matunda, kwani
nitamu na lenye ladha safi.Tunda hili husaidia
kulainisha ngozi ya uso iliyokauka, kwa mfano
utakuta kuna baadhi ya mafuta au losheni
zimecholwa ndizi.Kula ndizi ili urekebishe ngozi
ya uso wako pamoja na kuupa uwezo mzuri wa
ukumeng'enya chakula.
PAPAI: Ni tunda sahihi kabisa katika kukupa
ngozi yenye mafuta, kurudishia au kuziba
sehemu zilizoumia na kunyofoka katika ngozi
yako. Papai pia hunga'arisha rangi ya ngozi
yako, yote haya hufanyika na enzyme
inayotokana papai ambayo huitwa papain.
Endapo kama unataka kutumia papai katika
ngozi yako ya uso, basi chukua asali changanya
na papai lililo iva na paka usoni kwako kwa
dakika 10 kisha safisha, kisha utaona
kitakachotokea katika uso wako, utaonekana
kama ngozi ya mtoto wa siku mbili.
CHUNGWA: Hili ni chungwa maarufu sana
linalosaidia kurudishia ngozi iliyodhurika na
kuupa uhalisia wa ngozi yako. Jinsi ya kutumia
ni rahisi sana, chukua juisi ya chungwa ya baridi
kisha paka usoni, acha kwa dakika 10 kisha
osha utaona matokeo yake.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment