Baada ya taarifa za kutoweka, Kiongozi wa
chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe
ameibuka leo na kusema yuko salama wa afya
huku akilaani mbinu za Jeshi la Polisi kutaka
kumkamata kwa siri bila kufuata utaratibu
unaotakiwa.
Tangu Jumamosi usiku, vyombo mbalimbali vya
habari viliripoti Zitto kutofahamika alikokuwa
baada ya simu zake zote kutopatikana huku
viongozi wa chama hicho wakihofia kukamatwa
na polisi baada ya kubaini njia za uviziaji wa
kumkamata nyumbani
kwake.
"Ilikuwa Jumamosi , walikuja nyumbani kwangu
wakiwa na magari matatu ila hawakufanikiwa,
siwezi kukamatwa kwa `terms' zao ila nitakuwa
tayari kukamatwa kwa `terms' zetu na wala siyo
kuviziana, kama nina makosa kwa nini wanivizie,"
amesema Zitto Kabwe na kuongeza;
''Watu wetu wa Usalama wa Chama walihakikisha
kwamba sitakamatwa ili niweze leo kupata fursa
kuzungumza na watanzania kupitia nyie wana
habari
''Hatufahamu Watawala wanaogopa nini mpaka
kuzuia mikutano ya wanasiasa
''Nasikia Jana Walimkamata Mwenyekiti Mbowe wa
Chadema Huko Mwanza kisa eti kawasalimia
wananchi, huu ni uvunjwaji na ukiukwaji mkubwa
wa utawala wa kidemokrasia
''Tunalaani tabia za Kidikteta za Rais Magufuli
.Magufuli ameanza na vyama vya siasa kuonyesha
Udikteta wake, nawahakikishia akimalizana na
Vyama vya siasa atahamia kwenu Wanahabari,
Tumkatalie
''Ndio maana Magufuli Ziara yake ya Kwanza
alifanya Rwanda, tumegundua kuwa alikwenda
kujifunza namna ya Kudhibiti Demokrasia na
Kuongoza Kidikteta
''Hauwezi kupambana na Ufisadi kama haumpi
nguvu ya Kiutendaji wa CAG. Kwa hali Hii
anayokwenda Magufuli ajiandae kuwa rais wa
term moja kwa sababu watanzania hawataweza
kuvumilia kutawaliwa, kuminywa na kuburuzwa .
''CCM wamdhibiti Magufuli, na wasipomdhibiti sisi
na Watanzania Tutamdhibiti
''Hatutakaa Kimya hata kama atatufunga,
akimfunga Zitto watazaliwa wakina Zitto wengine,
na kwenye hili hatutakaa Kimya, tutasimama
kidete mpaka nchi irudi kwenye misingi''
''IGP ameagizwa na Magufuli anikamate, lakini
hawezi kunikamata bila kufuata utaratibu,
hawawezi kunikamata kwa kunivizia, viongozi
hatukamatwi kwa kuviziwa viziwa, tumewaonyesha
kwamba Polisi wanaweza kutukamata kwa kufuata
terms zetu na sio zao
''Karibuni kesho saa tisa kwenye Kongamano letu,
Hatuwezi kuacha kufanya siasa, lazima tuendelee
kufanya siasa, mmehudhuria mikutano yetu
hamjaona hata sisimizi amekanyagwa
''Wanasema Bajeti imeongezeka kwa 32% ukweli
ni kwamba Bajeti imeshuka kwa maana Dola
imeporomoka''
Home / Uncategories / BAADA YA KUTOWEKA KWA SIKU MBILI ZITTO AIBUKA NA HAYA HAPA SOMA UJUE ALICHOKISEMA
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment