Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba ametoa wito kwa Wananchi wa Kata ya Mbweni kutunza mazingira na kutoa kipaumbele kwa mazingira.
Mh. Makamba liyasema hayo wakati wa zoezi la upandaji mikoko lilifanyika katika fukwe za bahari ya Hindi zilizoko Mbweni.
Akiongoza Wananchi wa Kata hiyo kupanda miche 5,000 ya mikoko , Waziri Mkamba alisititiza pia wanafunzi wa shule waliopo katika eneo hilo kupenda mazingira yao na kuyatunza ili yawafae baadaye.
Wakisoma Risala yao, wanawake wa Mbweni walimuomba Waziri awasaidie kuwapatia vitendea kazi kwa ajili ya kuhudumia mikoko pamoja na kumuomba awasaide kuwatatulia changamoto wanazokutana nazo. Ikiwamo ya maafisa wa TRA kukata hovyo mikoko wanapokua wanafanya doria katika fukwe za Mbweni.
Aidha Waziri aliwahukuru wananchi wa Mbweni waliojitokeza kujumuika naye katika zoezi hilo la upandaji mikoko. Shughuli za upandaji mikoko ni kuelekea maadhimisho ya siku ya mazingira ambayo kilele chake ni Juni, 5 kila mwaka.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment