Comments


UVUTAJI SIGARA HADHARANI MARUFUKU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda amesema waendesha bodaboda na
abiria wasiovaa helmet watakamatwa na
kushtakiwa kwa kosa la kutaka kujiua.
Makonda aliyemwakilisha Makamu wa Rais
kwenye futari iliyoandaliwa na Benki ya NMB
kwa wateja na wadau wake juzi, alisema abiria
na wapanda vyombo hivyo wanatakiwa kuvaa
helmet.
Alisema kupanda pikipiki bila usalama ni
kwamba abiria anadhamiria kujiua, kwa sababu
akipata ajali ni rahisi kupoteza maisha kwa
kupiga kichwa chini.
“Nimeshawasiliana na kamati yangu ya usalama
barabarani mkoa, hili nitalisimamia kikamilifu
lazima wote wawe na helmet na wakikamatwa
wote watashtakiwa,” alisema.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kupanda bodaboda
bila kuvaa kofia hiyo, ni sawa na mtu
anayechukua vidonge na kunywa na pombe kali,
ambayo matokeo yake ni kifo.
Makonda alisema kazi hiyo ataifanya kipindi hiki
cha Mfungo wa Ramadhani ili apate thawabu
ikiwamo kuruhusu maduka makubwa kufanya
kazi hadi usiku wa manane.
Alisema hiyo itasaidia wanaofanya kazi wakirudi
nyumbani wanafuturu baadaye wanaswali
Tarawehe, hivyo wanaweza kwenda kufanya
manunuzi usiku.
Alisema kitakachofanyika ni kuimarisha usalama
wa raia kupitia kamati yake ya ulinzi na
usalama ya mkoa.
Pia, alisema atatangaza kupiga marufuku
uvutaji sigara hadharani zaidi kwenye
mikusanyiko na kupambana na vijana na watu
wanaojihusisha na uvutaji wa shisha (bangi).
“Mtu asiyevuta sigara, anakerwa sana na moshi
ndiye anayeathirika zaidi, nitatangaza rasmi hivi
karibuni marufuku ya kuvuta sigara, sasa watu
watafute kwa kuvutia… nitatangaza na hatua za
kuchukua,” alisema.
Makonda alitumia nafasi hiyo kuwataka NMB
kuchangia madawati, kwa shule za msingi na
sekondari katika mkoa wake.
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke
Bussemaker alisema utamaduni wa kufuturu
pamoja hasa katika Afrika unadumisha amani,
umoja na upendo miongoni mwa Waislamu na
watu wengine, hivyo wao wanauendeleza.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system