Comments


WANAFUNZI WAAMUA KUCHUKUA JUKUMU LA KIUALIMU MARA BAADA YA WAALIMU WAO KUACHA KAZI.

Wakazi wa kijiji cha Manga kilichopo kata ya
Mkata wilayani Handeni wameiomba serikali
kuingilia kati kufuatia walimu wawili wa shule
ya msingi Kwedichocho kuacha kazi tangu
mwishoni mwakajana na kuwaacha wanafunzi
wakifundishwa na wanafunzi wenzao wawili
wa darasa la saba kufuatia vitongoji vyao
pamoja na shule kuuzwa kwa mwekezaji
ikidaiwa kuwa ipo maeneo katika kijiji kingine
kinachojulikana kwa jina la Mazingara.
Wakizungumza katika kijiji cha Kwedichocho
baadhi ya viongozi wa serikali ya kijiji na
wakazi wake wamesema hatua hiyo imekuja
baada ya baadhi ya viongozi wa kijiji cha
Mazingara kumuuzia mwekezaji hekari zaidi
ya 400 zenye makazi ya watu zaidi ya 1000
pamoja na shule hatua ambayo wanafunzi
wameanza kutishiwa kuondoka kwa sababu
mwekezaji anataka kulifanyia kazi eneo la
ardhi ikiwa ni pamoja na majengo ya shule
pamoja na nyumba ya mwalimu.
Kwa upande wake mwenyekiti mstaafu wa
kijiji hicho Saleh Sadick amesema wakazi wa
vitongoji vya Kwedichocho na Mkulumilo
vyote vilivyopo katika kata ya Mkata
hawatakubali kuondoka katika eneo hilo
linalodaiwa kuwa ni eneo la kijiji cha
Mazingara hatua ambayo inaweza
kusababisha uvunjifu wa amani baina ya
pande hizo mbili.
ITV ilifika hadi katika shule ya msingi
Kwedichocho ambapo wananfunzi walikutwa
darasani wakifundishwa na wenyewe

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system