Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto
inaendelea na utaratibu wa kutoa taarifa
ya mwenendo wa mlipuko wa ugonjwa
Kipindupindu nchini kila wiki kama
tulivyoahidi, ili kutoa tahadhari kwa
wananchi na maelekezo ya hatua za
kuchukua ili kukabiliana na mlipuko huu.
Hadi kufikia tarehe 12 Juni 2016, jumla ya
wagonjwa 21,786 nchini wametolewa
taarifa,na kati yao Ndugu zetu 342
wamepoteza maisha tangu ugonjwa huu
uliporipotiwa Agosti 2015.
Takwimu zinaonyesha kuwa, katika wiki
hii inayoishia tarehe 12 Juni 2016, Idadi
ya wagonjwa walioripotiwa nchi nzima ni
78 na kati yao mmoja alipoteza maisha.
Wiki iliyotangulia kulikuwa na wagomjwa
62 waliotolewa taarifa na kati yao watatu
walipoteza maisha. Hii ikionyesha kuna
ongezeko la wagonjwa walioripotiwa wiki
hii ikilinganishwa na wiki iliyotangulia
ingawa kuna kupungua
Takwimu zinaonyesha kuwa, katika wiki
hii inayoishia tarehe 12 Juni 2016, Idadi
ya wagonjwa walioripotiwa nchi nzima ni
78 na kati yao mmoja alipoteza maisha.
Wiki iliyotangulia kulikuwa na wagomjwa
62 waliotolewa taarifa na kati yao watatu
walipoteza maisha. Hii ikionyesha kuna
ongezeko la wagonjwa walioripotiwa wiki
hii ikilinganishwa na wiki iliyotangulia
ingawa kuna kupungua
kwa Idadi ya waliopoteza maisha.
Mikoa iliyoripoti ugonjwa wa kipindupindu
wiki hii ni mitano(5), Morogoro ( wagonjwa
43 na kifo 1), Mwanza (21), Mara (7),
Lindi (4) na Manyara (3). Aidha wiki hii
wilaya zilizoripoti ugonjwa wa
Kipindupindu ni Morogoro vijijini
(wagonjwa 27 na kifo 1), Morogoro mjini
(8), Mvomero (8), Ilemela (12),
Nyamagana (9), Tarime vijijini (5), Tarime
mjini (2), Kilwa (4) na Simanjiro (3).
Mpaka sasa bado mikoa ya Njombe na
Ruvuma haijaripoti mgonjwa yeyote wa
Kipndupindu tangu mlipuko huu uanze
mnamo mwezi Agosti mwaka 2015
Licha ya kuwa kwa ujumla kasi ya
mwenendo wa ugonjwa wa kipindupindu
imekuwa ikipungua, takwimu hizi
zinaashiria kuwa ugonjwa wa kipindupindu
bado upo katika jamii tunazoishi na
unagharimu maisha ya watu ambao ni
nguvu kazi ya Taifa.
Hivyo wote kwa pamoja hatuna budi
kuendeleza juhudi za ufuatiliaji na
mapambano dhidi ya ugonjwa huu na
tuendelee kutekeleza na kusimamia
kikamilifu maelekezo na miongozo stahili
inayotolewa na Wizara yangu.
Wizara yangu inaendelea kutoa onyo kali
kwa Wasimamizi wa huduma za Afya
Mikoani na katika Halmashauri, ambao
wanaficha taarifa za wagonjwa wa
Kipindupindu. Yeyote atakayebainika kuwa
anaficha taarifa hizi atachukuliwa hatua
kali. Wizara yangu inasisitiza kuwa, juhudi
za kusimamia kikamilifu hatua mbalimbali
za udhibiti wa mlipuko huu ziendelee.
Aidha katika kipindi hiki ambapo ugonjwa
unaendelea kupungua,Wasimamizi wa
huduma za Afya Mikoani na katika
Halmashauri, waendelee kufuatilia na
kuchunguza kwa kina, taarifa zote za vifo
vinavyotokana na mgonjwa mwenye dalili
za Kipindupindu kama kuharisha na
kutapika. Taarifa hizi zinahitajika ili hatua
madhubuti za kuzuia vifo ziweze
kuchukuliwa.
Wizara inaendelea kuwapongeza na
kuwashukuru wadau wote kwa jitihada za
dhati zinazoendelea kutekelezwa na katika
kusimamia kikamilifu miongozo
inayotolewa na Wizara ili kuutokomeza
ugonjwa huu, ikiwa ni pamoja na
wataalamu wa sekta mbalimbali,
Mashirika ya Kimataifa, Watumishi, Mikoa
na Halmashauri pamoja na waandishi wa
habari na wananchi kwa ujumla.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment