Comments


MFAHAMU KOCHA MPYA WA PSG HUYU HAPA........

Unai Emery ameteuliwa kuwa Kocha Mpya wa Paris Saint-Germain, akichukua nafasi ya Laurent Blanc aliyeondoka Klabuni hapo mapema Wiki iliyopita.
Emery, mwenye Miaka 44, aliachana na Sevilla Wiki mbili zilizopita licha ya kuwa na Mkataba nao hadi Juni 2017.
Wakati PSG ikimthibitisha Emery, Sevilla nao wakatangaza kuwa Jorge Sampaoli, Kocha wa zamani wa Chile, ndie atakuwa Kocha wao mpya na kupewa Mkataba wa Miaka Miwili.
PSG waliamua kuachana na Blanc licha ya Kocha huyo kuwapa mafanikio makubwa Nchini France katika kipindi chake cha Miaka Mitatu ambacho alitwaa Ubingwa wa Ligi mara 3 na pia kuzoa Trebo mara 2.
Lakini Wamiliki wa PSG walichukizwa na udhaifu wa Timu yao kushindwa kuvuka hatua ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa Misimu kadhaa mfululizo.
Emery, ambae ni Kiungo wa zamani wa Real Spciedad, alianzia Ukocha akiwa na Valencia kati ya 2008 na 2012 na kisha kuhamia Sevilla Mwaka 2013 ambako alifanikiwa kutwaa UEFA EUROPA LIGI mara 3 mfululizo.
Emery amesaini Mkataba wa Miaka Miwili na PSG ukiwa na nyongeza ya Mwaka mmoja huku akitakiwa kuanza kazi mara moja.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system