Comments


PRF. MBARAWA ATOA AGIZO KWA TTCL

WAZIRI wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa
mwezi mmoja kwa Katibu Mkuu wa Wizara
anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano na
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu nchini
(TTCL), kuhakikisha kituo cha kutunzia taarifa
(Data Centre) kilichopo Kijitonyama jijini Dar es
Salaam kinaanza kufanya kazi.
Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo kufuatia
kukamilika kwa Data Centre hiyo miezi kadhaa
iliyopita na mahitaji ya wadau wa huduma ya
kutunza kumbukumbu za taasisi zao katika kituo
hicho kuongezeka.
“Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano na
Mtendaji mkuu wa TTCL hakikisheni kituo hiki
kilichojengwa kwa gharama kubwa kinaanza
kutumika na kuwezesha mashirika na taasisi
mbalimbali kutunza kumbukumbu zao na kuiletea
Serikali mapato”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Prof. Mbarawa amesema huduma ya mtandao
katika kituo cha Data Centre imeimarishwa
kutokana na kuunganishwa na Mkongo wa Taifa
wa Mawasiliano hivyo itawarahisishia wateja wake
kuweka na kuchukua taarifa zao kwa haraka.
Akizungumza mara baada ya kukagua maeneo
mbalimbali unapopita Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano Prof. Mbarawa amemtaka
Mkurugenzi wa TTCL kanda ya Kaskazini Bw.
Peter Lusama kuhakikisha Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano unapitishwa juu ya nyaya katika
maeneo yenye changamoto za mafuriko ili
kuepuka uharibifu wa mara kwa mara na
usumbufu kwa watumiaji.
Aidha amezitaka taasisi za Serikali na binafsi
kukitumia kituo cha kisasa cha kuhifadhi taarifa
DATA CENTRE kutunza taarifa zao ili
kuzihakikishia usalama na uhakika wa kuzitumia
wakati wote, ambapo asilimia 75 imetengwa kwa
ajili ya kutunza taarifa kutoka sekta binafsi na 25
itatunza taarifa za Serikali.
Kituo hicho ambacho ni cha kwanza kujengwa
katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati
ni fursa mpya kwa wafanyabiashara na wadau
mbalimbali wenye taarifa nyingi kuzihifadhi na
kuzitumia wanapozihitaji kinamilikiwa na Serikali
na ujenzi wake umegharimu takribani dola za
kimarekani milioni 93.
Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua
uwanja wa ndege wa Singida na mahali
utakapojengwa uwanja mpya na kusisitiza
umuhimu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
nchini kusimamia kikamilifu ujenzi wa uwanja wa
ndege wa sasa ambao upembuzi yakinifu wake
umekamilika.
Amesema tayari Serikali imebainisha viwanja 11
vya ndege nchini kote na kuvifanyia upembuzi
yakinifu kabla ya kuanza kuvijenga ili viweze
kukidhi mahitaji ya soko.
Amevitaja viwanja hivyo kuwa ni Lake Manyara,
Musoma, Iringa, Tanga, Songea, Kilwa Masoko,
Lindi, Moshi, Njombe, Simiyu na Singida ambavyo
vitapanuliwa na kujengwa kwa kiwango cha lami.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system