Wabunge wa chama cha mapinduzi CCM ndani ya bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, wamesema wanashangazwa na maamuzi ya kambi ya upinzani bungeni kuamua kususia vikao vya bunge vinavyoendeshwa na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson,kwa kusema kuwa Naibu huyo spika anaendesha vikao hivyo kwa mujibu wa katiba za uendeshaji wa bunge.
Taarifa hiyo ya wabunge wa CCM,iliyoongozwa na naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri Mkuu, Dkt Abdallah Possi,imetolewa katika mkutano wa waandishi wa habari mara baada ya vikao vya bunge kumalizika, huku mbunge wa jimbo la Mwibara Kangi Lugola akiwanyoshea kidole maafisa wa wizara ya elimu.
Awali katika kipindi cha maswali na majibu serikali imeliambia bunge kuwa haitarudi nyuma kuhusu uamuzi wake wa kuzima simu feki ifikapo june 16, huku ikizitaja sababu za kiafya na kiusalama kama moja ya sababu kuu za kuzima simu hizo.
Wakati Tanzania ikiungana na nchi zingine duniani kuadhimisha siku ya mazingira yaliyoanza June mosi hadi June tano, serikali kupitia wizara ya makamu wa Rais Muungano na mazingira imesema kuanzia Julai mosi imetenga fedha kwa ajili ya kusambaza miche ya miti katika halmashauri mbalimbali nchini.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment