Comments


DAWASCO WADHIBITI UPOTEVU WA MAJI.

SHIRIKA la majisafi na majitaka Dar es
Salaam (DAWASCO), limefanikiwa
kupunguza kiasi cha upotevu wa maji
kutoka asilimia 61 hadi kufikia 47 huku
ikiwa na mpango wa kufikisha asilimia 45
mwisho mwa mwezi juni.
Akizungumza wakati wa oparesheni
maalumu ya kudhibiti mabomba ya maji
yanayovujisha maji pamoja na
kuwaunganishia maji wateja wake
waliokatiwa maji kutokana na madeni
Sinza Dar es Salaam jana, Afisa Mtendaji
Mkuu wa Dawasco, Cyprian Luhemeja
alisema wameamua kuingia mtaa hadi
mtaa kukabiliana na tatizo hilo.
“Shirika limedhamiria kwa dhati
kukabiliana na tatizo la upotevu wa maji,
unaotokana na uchagavu wa miundombinu
ambapo hadi sasa tumefanikiwa
kupunguza tatizo hilo kutoka asilimia 61
ya awali hadi kufikia 47 ya sasa,” alisema
Luhemeja.
Luhemeja alisema shirika limekuwa
likiingia gharama kubwa ya kutibu maji
kwa dawa lakini maji hayo yamekuwa
yakiishia njia kutokana na uchakavu wa
miundominu hivyo sasa wameamua
kulivalia njuga tatizo hilo na kulimaliza
kabisa.
Aidha mbali na udhibiti huo wa maji
yanayovuja njiani pia Luhemeja alisema
Dawasco imeamua kuwarejeshea wateja
wake waliokatiwa maji kutokana na
madeni ya muda mrefu na kukubaliana
namna ya kulipa madeni hayo huku
wakiendelea kupata huduma.
“Tunawateja wengi ambao walikatiwa maji
kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja
na madeni tunawataka waje katika ofisi
zetu za kanda zilizo karibu nao ili waweze
kurejeshewa maji na kupangiwa utaratibu
wa kulipa madeni yao,” alisema Luhemeja.
Wakiwa katika kazi hiyo ya kuunganishia
watu maji na kutengeneza mabomba ya
maji yanayovuja mtaa wa Sinza E Dar es
Salaam, Afisa Mtendaji huyo alitoa ofa ya
kumrejeshea huduma ya maji mama mjane
Asha Mohamed mkazi wa Mtaa wa Ngamia,
Sinza ambaye alikatiwa maji tangu mwaka
2002 kwa kudaiwa bili ya maji ya sh
200,000.
Akizungumza kwa furaha ya kurejeshewa
maji Asha Mohamed, ameishukuru
Dawasco kumrejeshea maji na kuahidi
kulipa bili zake kwa wakati.
Nae Mwenyekiti wa Mtaa huo wa Sinza E,
Kassim Kabulluh, alisema eneo lake likuwa
likikabiliwa na kero ya uvujishaji maji
barabarani jambo ambalo lilikuwa
likiharibu miundombinu ya barabara.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system