Comments


KAMPUNI ZA SIMU ZAPEWA MWEZI MOJA KUPELEKA HUDUMA ZA MAWASILIANO VIJIJINI

3 (2)Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa kampuni za simu  nchini zilizoingia makubaliano na Serikali kupeleka huduma ya Mawasiliano vijijini  kukamilisha kazi hiyo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo  mkoani Iringa  mara baada ya kukagua  mitambo ya kampuni ya simu ya (TTCL) na kubaini kwamba bado kuna baadhi ya  vijiji havijafikiwa huduma ya mawasiliano  licha ya mkataba wa kutekeleza kazi hiyo  kati ya serikali na kampuni hizo kusainiwa miaka miwili iliyopita.


Kuhusu suala la kukatwa kwa mkongo wa taifa wa mawasiliano  katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Iringa Prof. Mbarawa amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa mtu au taasisi  itakayoharibu miundombinu hiyo.

Aidha, amemuagiza meneja wa TTCL mkoa wa Iringa Eng. Ekael Manase kuhakikisha kuwa minara iliyojengwa katika maeneo ya vijiji Mkoani humo inaanza kutoa huduma ya mawasiliano kabla ya mwisho wa mwezi huu.

Katika hatua nyingine Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amekagua barabara ya Iringa-Kalenga hadi Hifadhi ya Taifa ya Ruaha yenye urefu wa KM 134 ambayo usanifu wake umekamilikka na kusisitiza kuwa itajengwa kwa kiwango cha Lami.

Naye Mbunge wa Isimani ambaye ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Willium Lukuvi amesema ujenzi wa barabara hiyo ukikamilika utafufua uchumi wa Mkoa wa Iringa kwa kuwa utavutia wawekezaji na watalii katika Hifadhi ya Ruaha.

Prof. Mbarawa yuko katika ziara ya siku nne katika Mkoa wa Iringa ya kukagua maendeleo ya Miundombinu ikiwa ni mkakati wa Serikali kufufua uchumi wa Mkoa huo.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system