Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
tarehe 13 Juni, 2016 amewaapisha
mawaziri wawili kufuatia mabadiliko
madogo ya Baraza la Mawaziri
aliyoyafanya Jumamosi tarehe 11 Juni,
2016.
Mawaziri walioapishwa leo Ikulu Jijini Dar
es salaam ni Mhe. Mwigulu Lameck
Nchemba aliyeapishwa kuwa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye
ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi
anakwenda Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, akitokea Wizara ya Kilimo, Mifugo
na Uvuvi.
Waziri mwingine ni Dkt. Charles John
Tizeba ambaye ameapishwa kuwa Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Dkt. Charles John Tizeba ambaye ni
Mbunge wa Jimbo la Buchosa aliteuliwa na
Rais Magufuli kuwa Waziri wa Kilimo,
Mifugo na Uvuvi kuanzia tarehe 11 Juni,
2016.
Hafla ya kuapishwa kwa Mawaziri hao
imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe.
Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu
Mhe. Kassim Majaliwa.
Imetolewa na :
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,
IKULU Dar es salaam, Gerson Msigwa
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment