Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ameagiza
hospitali zote za Serikali kuwa na kibao
kilichoandikwa ‘Damu ni bure na haiuzwi’, katika
jitihada za kuondoa urasimu wa upatikanaji wa
damu kwa wahitaji.
Ummy amesema hayo alipokuwa anazungumzia
maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu
Duniani, inayoadhimishwa duniani kote kila
ifikapo Juni 14, lengo likiwa kukusanya damu na
pia kuwaenzi watu ambao wamekuwa
wakichangia damu kwa hiyari na kuokoa maisha
ya wahitaji.
Alikemea tabia ya baadhi ya watumishi wenye
urasimu katika utoaji damu na hata kusababisha
mazingira ya rushwa, huku akisisitiza lazima
damu itolewe bure kwa wananchi.
“Tanzania inahitaji chupa 450,000 za damu kwa
mujibu wa maelekezo ya Shirika la Afya Duniani
(WHO), huku akifafanua kuwa, mahitaji ya damu
katika kila nchi ni asilimia moja ya idadi ya raia
wake,” amesema.
Pamoja na agizo hilo, amefafanua kuwa ndugu
wa mgonjwa wanaweza kutoa damu kwa hiyari,
huku akisema kuna wakati makundi fulani ya
damu yanakosekana hivyo isitafsiriwe kuwa ni
urasimu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment