Comments


QUARESMA AIUA CROATIA NA KUIFANYA URENO KUPETA ROBO FAINALI


Add caption


Mchezaji wa Croatia Perišić’s ambaye alikuwa kivutio kwa mtindo wa nywele zake. Hata hivyo katika mchezo huo wa leo,licha  ya kutegemewa timu yake imeshindwa kufurukuta na kuambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Ureno
Mchezaji wa Ureno, Renato Sanches ambaye pia ni mchezaji bora wa mchezo huo akijaribu kumtoka mchezaji wa Crotia
Mchezo baina ya timu ya Taifa ya Croatia dhidi ya timu ya Taifa ya Ureno katika michuano ya Uefa Euro 2016, umemalizika kwa timu ya Ureno kusonga mbele  kwa ushindi wa bao 1-0.
Awali mchezo huo ulimalizika kwa dakika 90 za mchezo kwa kutoka 0-0 na kuingia hatua ya pili ya lala salama ambazo ziliongezwa dakika 30. Mchezo huo uliokuwa mkali kwa pande zote mbili, Croatia watajijutia wenyewe kwa kukosa nafasi nyingi lakini Ureno walitumia nafasi hiyo ya kipekee na
kuweza kupachika bao hilo ambalo lilitafutwa kwa taabu na mchezaji nyota wa timu hiyo, Christian Ronaldo ambaye pia alipiga shuti lake na kuokolewa na kipa wa Croatia na mpira huo kuja kumpata mchezaji huyo wa Ureno aliyetokea benchi, Quaresma na kupachika bao hilo kwa kichwa na kufanya mchezo huo kuwa Croatia 0-1 Ureno.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system