Comments


MAN UNITED YAPOKONYWA TONGE MDOMONI DK Ya 90



Mechi za Ligi Kuu Uingereza zimeendelea usiku wa January 12, kwa vilabu vyaMachester United kuwa mgeni wa Newcastle United katika dimba la St James’ Park, wakati Bournemouth walikuwa wenyeji wa West Ham United na na Aston Villa wenyeji wa Crystal Palace.
301A3E8400000578-3396245-image-a-5_1452636672481
Mchezo wa Man United ndio mchezo ambao ulikuwa unapewa nafasi kubwa ya kutazamwa na watu wengi zaidi, kwani timu hiyo ina wapenzi wengi na kocha wake Louis van Gaal amekuwa kwenye headlines za kuhusishwa kufukuzwa kila siku kutokana uongozi kudaiwa kutoridhishwa na kiwango cha timu yake.
301A3A5F00000578-3396245-image-a-96_1452634838972
Mchezo huo ulimalizika kwa Newcastle United kutoka sare ya goli 3-3 na Man Unitedkatika uwanja wake wa nyumbani, hayo yalikuwa matokeo ambayo yaliwashangaza wengi, hususani mashabiki wa Man United kwani hadi dakika ya 89 walikuwa mbele kwa goli 3-2, hivyo goli la dakika ya 90 la Paul Dummett lilivunja nguvu na kuishangaza Man United.
3444
Magoli ya Man United yalifungwa na Wayne Rooney kwa mkaju wa penati dakika ya 9, na dakika ya 79 akafunga goli la tatu, baada ya Jesse Lingard kupachika goli la pili kwaMan United dakika ya 38. Magoli ya kusawazisha ya Newcastle United yalifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 42, Aleksandar Mitrovic dakika ya 67 na Paul Dummett dakika ya 90, nakufanya Man United iliyokuwa na matumaini ya kuvuna point tatu hadi dakika ya 89, kuambulia point moja pekee.
Video ya magoli ya Newcastle United Vs Man United
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system