Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein, amesema serikali yake itaendelea kuchukua hatua za makususdi katika kuhakikisha sekta ya elimu inaimarika.
Akizungumza mwishoni mwa wiki visiwani humo wakati akipokea msaada wa madawati 50 kutoka kwa Masheikh wa Jumuiya ya Khoja Shia Ithna Sharia amesema kuwa SMZ inathamini sekta ya elimu ndio maana ilianza kutoa elimu tangu wakati wa Hayati Abeid Amani Karume.sheinRais Shein amesema katika kuimaarisha sekta hiyo wananchi na taasisi mbalimbali wanapaswa kujitokeza kuiunga mkono sera ya elimu bure ili izidi kuimarika.
0 comments:
Post a Comment