Mmoja wa washambuliaji wa kujitoa mhanga waliohusika katika shambulio lililotekelezwa karibu na kambi ya vikosi vya Umoja wa Afrika (AU) mjini Mogadishu mnamo Jumanne aliwahi kuwa mbunge.
Salah Nuh Ismail, 57, alikuwa miongoni mwa watu 13 waliofariki kwenye milipuko miwili iliyotokea karibu na uwanja wa ndege, kundi la al-Shabab lilisema.
Alijulikana sana kama Badbado, jina ambalo maana yake ni ‘Usalama’ au ‘Yule Salama’.
Alijiunga na Bunge la Somalia mwaka 2000 lakini akajiuzulu na kujiunga na al-Shabab mwaka 2010.
Anakumbukwa sana kwa kuwaita wabunge wenzake “makafiri”, baada yake kujiunga na kundi hilo la Kiislamu.
Kambi kuu ya Amisom yavamiwa Mogadishu
Alipokelewa kwa heshima kubwa na maafisa wakuu wa kundi hilo ambao walisema “alijutia makosa aliyokuwa ameyatenda”.
Washambuliaji wawili wa kujitoa mhanga walihusika
Tofauti na washambuliaji wengine wa kujitoa mhanga, ambao huwa vijana na watu wasiosoma sana na ambao si maarufu, yeye alikuwa mtu mzee kwa umri, aliyeelimika na mtu maarufu.
Al-Shabab wamekuwa wakikabiliana na serikali ya Somalia ambayo huungwa mkono na Umoja wa Afrika na jamii ya kimataifa.
Eneo la karibu na uwanja wa Mogadishu hulindwa sana na hutumiwa kwa shughuli za Umoja wa Mataifa.
Mataifa mengi yana afisi za kibalozi eneo hilo.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment