Comments


waziri mkuu kasimu majaliwa asema serikali itajenga viwanda vya kutosha.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema
Serikali itahakikisha viwanda vinajengwa kwa
wingi nchini kwani ndiyo msingi imara wa ukuaji
wa uchumi na muarobaini wa tatizo la ajira
hususan kwa vijana.
“Mbali na kukuza uchumi na kuongeza fursa za
ajira nchini, viwanda hivi ndivyo vitakavyotufanya
tununue bidhaa kwa bei nafuu tofauti na ilivyo
sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje
ya nchi,” alisema.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumatano
Julai 13, 2016) wakati akikagua ujenzi wa
kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha
Goodwill Tanzania Ceramic katika kijiji cha Mkiu
wilayani Mkuranga, Pwani.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
kiwanda hicho Bw. Frank Yang alisema jumla ya
ajira 4,500 zinatarajiwa kutolewa kiwandani
hapo mara ujenzi utakapokamilika.
Akifafanua kuhusu ajira hizo Bw. Yang alisema
ajira 1,500 zitakuwa rasmi na zisizo rasmi
zitakuwa 3,000 huku wakazi wanaoishi katika
maeneo yanayozunguka kiwanda hicho
wanatarajiwa kupewa kipaumbele. Mkurugenzi
huyo alisema ujenzi wa kiwanda hicho
utagharimu dola milioni 100 na utafanyika kwa
awamu mbili. Awamu ya kwanza inatarajiwa
kukamilika Desemba mwaka huu.
“Ujenzi wa kiwanda hiki utainua ukuaji wa uchumi
nchini Tanzania kwani utakapokamilika Serikali
itakusanya sh. bilioni 30 kwa mwaka ikiwa ni
mapato ya kodi,” alisema.
Naye Balozi wa China nchini Tanzania Dk.Lu
Youqing aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa
kuchagua sekta ya viwanda kuwa ndiyo
kipaumbele chake katika kukuza uchumi.
Alisema mbali ya ujenzi wa kiwanda cha vigae
katika eneo hilo pia wawekezaji hao kutoka
nchini China wanatarajia kujenga viwanda vya
mbolea, karatasi na glasi (bilauli).
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alipokea
msaada wa madawati 500 yenye thamani ya sh
milioni 40 ambayo yalitolewa na Balozi wa
China nchini Dk. Lu kwa kushirikiano na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Goodwill
Tanzania Ceramic Bw. Yang.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system