Jiwe kubwa au dogo linaweza kutumika katika mambo
mengi, zamani wazazi wetu waliyatumia kusagia nafaka, na hata wahunzi
walichonga nyenzo mbalimbali za kutumia kama majembe, mapnga, visu na
mikuki kwa kutumia mawe.
Leo
hii katika maeneo mbalimbali ya nchi ambayo yanapatikana mawe mazuri na
kama kuna wajenzi wa barabara au majumba utaona kuna mashine za
kupasulia kokoto katika maeneo hayo.
Ndugu
zetu wa china wao wamefika mbali mawe yetu hasa pale Msolwa Mkoani
Pwani/Morogoro wanayakata kwa ufundi na kutoa vigae vya sakafu na
ukutani "tails' ambazo huzisafirisha kwenda kwao na kunakishiwa vizuri
na kisha kurejeshwa hapa kwetu vikiwa vimeongezwa thamani kwa kuwekwa
kwenye boxi zuri na kuvinunua kwa bei ya juu hii nayo ni THAMANI YA
JIWE.
THAMANI
YA JIWE! Hapa natumia jiwe hili kuwaeleza ni kwa jinsi gani msanii huyu
ameweza kunipa somo mimi binafsi na sasa naamua kuwapa kile ambacho
nimekielewa mimi kutokana na JIWE hilo na Msanii huyu.
Jiwe
kama jiwe ni sawa na rasilimali nyingi ambazo watanzania katika nchi
Yetu nzuri tumejaliwa kuwa navyo, Nchi imejaliwa kwanza watu wazuri na
hodari waliona uwezo wa kujibidisha na kujitafutia ridhiki, pia nchi
inao watu wabunifu na wasomi wa nyanja mbalimbali na wengi wao kwa sasa
ni vijana walio na elimu na nguvu.
Lakini
pia nchi yetu Tanzania imejaliwa rasiliamali Ardhi iliyo na Madini,
yenye thamani kubwa zaidi duniani japo yapo ardhini. Lakini pia tuna
mito, maziwa na mabwawa mengi ambayo yamejaaliwa maji yakutosha. Hizi ni
fursa.
Jitihada
na bidii binafsi ndicho kitu pekee nadhani tumekikosa pamoja na ubunifu
wa kutumia fursa zilizopo kubadili maisha yetu hasa vijana ndicho kitu
ambacho tumekikosa licha ya wengi wetu kuwa na elimu ya darasani na ile
ya mtaani.
Tuwe
wabunifu wakuona kwanza vitu vilivyotuzunguka kama ni moja ya fursa na
tunapaswa kuzichangamkia ii zitutoe kimaisha. Hebu tuanze kuongeza
thamani ya rasilimali tulizo nazo. Fikiria tu kipande cha ardhi ambacho
unaweza kulima kwa kufuata utaalam wa kisasa na kuweza kujipatia mavuno
bora na kuweza kupata kipato zaidi ya mwajiriwa.
Kwakutumia
kipande kidogo cha ardhi unaweza kufuga, kuku wa kienyeji na hata
samaki na kujipatia kipato mara dufu. Tumekosa tu kujiongeza! Kubuni na
kufanya kazi kwa bidii kama ambavyo tunaona Msanii huyu Mzungu anavyo
chonga jiwe na kuliongeza thamani mara dufu.
JIWE
ambalo labda ungeweza kuliuza kwa mponda kokoto kwa sh 10,000 sasa
linaweza kuuzwa hata Milioni 5. Sijui wewe msaanii wa uchongaji uliyopo
Singida, Iringa, Morogoro, Kigoma na Mwanza au Kagera ambaye unalia
hakuna tena miti ya Mpingop ya kuchonga vinyago, ilhali umekalia jiwe
ambalo ni imara kuliko Mti wa Mpingo ambao ni nyara ya taifa kwa sasa
unajisikiaje.
Yes!
Umekalia Jiwe unawaza hakuna miti ya Kuchonga vinyago. Hahahaa Umekalia
uchumi, nyanyuka, kuwa mbunifu na sasa kamata fursa hiyo ya Mawe
yachonge sanamu kubwa kwa ndogo na utaona faida yake.
Anza
sasa kutumia fursa uiyonayo na kipaji ulicho jaaliwa na Mungu kwa
kuinua maisha yako. Utaliaje huna hata shiingi ilihali nyumbani kuna
eneo unaweza hata kulima mchicha? Mboga mboga zinalipa na wala
haziihitaji eneo kubwa.
Kwanini
unapanda maua kuzunguka nyumba na unayamwagilia maji kila siku ilhali
unaweza kupanda spinachi katika makopo yako hayo na kuwauzia majitrani
na kupata fedha na huku nyumbani kwako pakawa bado panaonekana kwa
kijani.
Halafu
kijana unatembea na vyeti na kubadili bahasha kila kukicha na kusaka
ajira. Huenda hata wazazi wako wanasikitika kujenga jumba kubwa lakini
unashindwa kulitumia kwa kupanda mbogamboga.
Vijana
ndio taifa a leo hapa Tanzania, tukiweza kujituma kwa bidii hakika
matunda tutayaona muda si mrefu. Wasiliana na wenzako ambao mlikutana
shule aidha sekondari au Vyuoni na kuwauliza huko wanakotoka kuna fursa
gani? Maana leo mimi natoka Kinyenze, Pale Mvomero Mkoani Morogoro,
tumejaliwa kuwa na ardhi walau heka tano na wewe mwenzangu umetokea
Masaki au Oysterbay jijini Dar es Saaam, Mzazi wako anaweza kukupa Sh
1,000,000/= kama mtaji na ukaja na pampu tu ya maji na pembejeo nyingine
hapa Kinyenze na tukalima mboga mboga maana mimi nilikosa mtaji na
baada ya mwezi tunafika mbali.
Tufikirie
kujiajiri zaidi Tuongeze Thamani ya JIWE letu ambalo ama ni akili zetu
au Ardhi na Chochote tulicho nacho na hakika tutaweza kujikwamua.
Tusitumie mawasiliano kwa kupeana taarifa tu za C & P.
Tukifanya
kazi kwa nidhamu na utuivu kama ambavyo msaanii huyu anaechonga jiwe
hili itaweza kutupa faida sana na wengi wakavutiwa na sisi na kutuiga.
Utakapo
anza kazi usikate tamaa fanya kazi kwa bidii hata watu wakisema vipi
wewe songa mbele na daima mtafutaji hachoki na akichoka kapata.
Tumia
kila anina ya nyenzo ulizonazo katika kufikia malengo yako. Amini kuwa
elimu au ujuzi uionao unatakiwa tu kutumika na mtu mwingine na kujipatia
kisha yeye afikirie namna ya kukulipa. AJIRA NI UTUMWA. Jiajiri kutumia
fursa zilizo kuzunguka ili ujikomboe katika Utumwa huo.
Hadithi
hii ya JIWE LILILOONGEZWA THAMANI binafsi imenipa somo kubwa sana,
nahata wewe naamini imekupa somo, kuwa kumbe inawezekana kutumia kitu
fuani kubadilisha na kuwa cha namna ingine na kizuri zaidi.
Kuwa
Smart katika maamuzi yako na uyaheshimu maamuzi hayo kwa kuyafanyia
kazi. Usikubaliwa kuyumbishwa na vitu ambavyo naweza kuvifananisha na
vumbi. Ona Msanii wetu licha ya vumbi la msasa lakini amevaa nguo
nyeupe. Jitose kulima au kufuga na kufanya kazi halali bila kujali
kiwango cha elimu ulicho nacho kuwa watu watakuonaje.
Binafis
nakumbuka miaka ya mwanzoni ya 2000 licha ya kuwa na Diploma yangu ya
Uandishi wa habari lakini nilikuwa nimejibidisha sana katika kilimo
nikiwa pale Kibaha. Nikilima Mahindi chini ya Nguzo za Umeme za Gridi ya
Taifa, nililima zaidi ya Heka mbili na nilihudumia vizuri shamba lile
na kila aliyepita alitamani liwe lake.
Sikuwa
na muda wa kukaa vijiweni labda usiku kuanzia saa moja huko ili nijue
tu kunanini duniani. Nakumbuka Mwalimu mmoja aliyekuwa akifundisha Chuo
fani maeneo yale akikaa Mwanalugali aliniita asubuhi moja na kuniuliza
vitu kutokana na jinsi ninavyo jituma akaniambia anatamani vijana wake
nao wawe kama mimi maana wakwake wamemaliza kidato cha nne tu lakini
wanajiona wasomi hawayaki kujituma kufanya chochote akini mimi na
Diploma yangu nilisha jembe.
Hivyo
usidhani kama elimu uliyonayo na ujuzi ulio nao kama utautumia kwa
kutembea na vyeti tu mkononi vitaleta tija. Bali tuamke sasa na kutumia
fursa zinazotuzunguka. Inawezekana sijasema kia kitu lakini nimegusia tu
namna gani unaweza kutumia fursa uiyonayo kwa vitu ulivyonayo katika
mazingira yetu tunayoishi. Usibaki kama Jiwe. Ambalo lenyewe haliwezi
kujibadili hadi libadilishwe, sasa wewe usingoje kuwa jiwe kwa
kubadiishwa na kuwa kitu fulani.
Jiwe Lililoongezwa Thaani...
0 comments:
Post a Comment