Msimu wa 2016/2017 unataraji kuanza hivi karibuni mwezi ujao na tayari vilabu mbalimbali nchini Uingereza vimeshaonyesha mwonekano wa jezi ambazo watazitumia msimu huo pamoja na namba za jezi ambazo zitatumiwa na wachezaji wapya wa timu hizo.

Manchester United ni moja ya timu ambazo zimetoa orodha ya namba ambazo watatumia wachezaji wake kwa msimu wa 2016/2017 na katika jambo ambalo halijawashangaza wengi ni kumpa mshambuliaji mpya wa klabu hiyo, Zlatan Ibrahimovic jezi namba 9 ambayo ukitoa jezi namba 7 inafuatia kwa heshima katika klabu hiyo.

Baadhi ya mastaa waliowahi kutumia jezi hiyo ni pamoja na Brian McClair, Andy Cole, Andrew Cole na Louis Saha.

Uwezo wa wachezaji ambao waliwahi kuitumia jezi hiyo wanaifanya kuwa na heshima na hivyo mchezaji ambaye anapatiwa jezi namba 9 anakuwa na jukumu kubwa la kuhakikisha anapachika magoli mengi ili kuiwezesha timu hiyo kutwaa makombe mengi kama jinsi ilivyokuwa imezoeleka.