Baadhi ya wakazi wa Mji wa Kibaha wakipata huduma ya upimaji wa macho na miwani bure katika kituo cha afya mkoani kutoka kwa madaktari bingwa raia wa Marekani ,mpango ambao umeratibiwa na mbunge wa Jimbo la Mji wa Kibaha Sylvestry Koka.
Mbunge wa Jimbo la Mji wa Kibaha Mjini, Sylvestry Koka akizungumza na madaktari bingwa wa magonjwa ya macho na kinywa kutoka nchini Marekani katika kituo cha afya cha mkoani,muda mfupi kabla ya wataalamu hao kuanza kutoa huduma ya upimaji macho na ugawaji wa miwani bure mpango ambao umeratibiwa na mbunge huyo .
ZAIDI ya wakazi 10,000 katika Mji wa Kibaha mkoani Pwani,wanatarajiwa kupata huduma ya tiba ya macho,miwani na kinywa bure katika kituo cha afya Mkoani kwa muda wa siku mbili .
Tiba hizo zinatolewa bure chini ya mpango ulioratibiwa na mbunge wa jimbo la mji wa Kibaha Silvesrty Koka pamoja na madaktari bingwa kutoka nchini Marekani .
Awali akizungumza kabla ya kuanza kwa zoezi hilo juzi,Koka alisema lengo lake ni kuwasaidia wananchi wanaosumbuliwa na matatizo hayo katika jimbo hilo.
Aidha alielezea kuwa mbali ya tiba hizo kutolewa bure pasipo malipo pia jumatatu (July 4)baadhi ya wauguzi pamoja na baadhi ya madaktari watapatiwa mafunzo mbalimbali juu ya tiba za macho yatakayowawezesha kuendelea kutoa huduma hiyo kwa wananchi.
“Natambua juhudi za serikali katika kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora hivyo nikaamua kuwaomba wataalamu wa magonjwa hayo nchini Marekani kuja kusaidia kutoa huduma hizi”
“Falsafa ya “hapa kazi tu” haiwezi kutekelezwa endapo hakuna mwenye kuwa na afya nzuri,hivyo imani yangu ni kuwa baada ya wananchi waliokuwa na matatizo ya kiafya ikiwemo macho na meno watakapopata huduma hii watatekeleza kwa vitendo agizo la Raisi John Magufuli la kufanyakazi”alisema Koka.
Koka alielezea kuwa afya ni kitu muhimu kwa binadamu kuliko kitu chochote hata mali kwani unaweza kuwa na utajiri mkubwa lakini kama huna afya bora huwezi kufanya lolote.
Alisema ni jukumu lake kusimamia kero mbalimbali zinazowakabili wananchi wa jimbo lake katika sekta mbalimbali ikiwa ni sanjali na afya,elimu,miundombinu na mengineyo mengi.

Hata hivyo Koka alisema ataendelea kuzitafutia ufumbuzi kero zinazokabili sekta ya afya ili kuwaondolea adha wananchi jimboni hapo.
Kwa upande wake daktari wa macho katika kituo cha afya mkoani ,Makonde Kilumbi alisema kumekuwa na ongezeko la idadi ya wagonjwa wanaosumbuliwa na tatizo la macho na ugonjwa wa presha ya macho .
Alisema ugonjwa wa presha ya macho kwa sasa umekuwa ni tatizo linalowakumba watu wengi na ugonjwa wa mtoto wa jicho ambapo wamekuwa wakipokea wagonjwa 150 hadi 200 kituoni hapo.
Dk.Kilumbi alisema chanzo kikubwa cha matatizo ya macho ni vumbi,mazingira machafu na hali ya kijiografia.
Akizungumza kwa niaba ya Madaktari kutoka nchini Marekani, mmoja wa wataalamu hao,Profesa Conrad Shayo alisema kutokana na hali halisi waliyoiona kuna kila sababu ya serikali kuweka mkakati mathubuti wa kukabiliana na matatizo hayo.
Baadhi ya wakazi waliofika kupata huduma hizo,akiwemo Nancy Godfrey,Cecilia Kimario walimshukuru Koka kwa kuwezesha mpango huo kuwafikia kwani wengi wao wanasumbuliwa na tatizo hasa la macho.

Mgeni Msafiri alimpongeza mbunge huyo na kuomba aendelee kusimamia changamoto zinazokabili vituo vya afya,zahanati jimbo humo ikiwa ni pamoja na madawa na vifaa tiba.
Mgeni alisema sekta ya afya bdo ina changamoto nyingi hivyo kuna kila sababu ya kupigania kero zilizopo ili ziweze kupungua kama sio kumalizika na kubaki historia.
0 comments:
Post a Comment