Comments


Lionel Messi kahukumiwa miezi 21 jela kwa kosa la ukwepaji kodi

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina anayeichezea klabu ya FC Barcelona yaHispania Lionel Messi, leo July 6 2016 jina lake limeingia kwenye headlines baada ya hukumu ya kesi yake ya ukwepaji kodi kutoka.
Lionel Messi amehukumiwa miezi 21 jela kutokana na kosa la ukwepaji kodi, hukumu hiyo ya Lionel Messi imetoka kutokana na kosa la kutuhumiwa kukwepa kodi pamoja na baba yake mzazi Jorge Messi kati ya mwaka 2007 na 2009, kiasi cha dola milioni 4.5 ambazo ni zaidi ya Tsh bilioni 9.8.
Hata hivyo kwa mujibu wa sheria za Hispania kwa watu wanaohukumiwa kifungo cha chini ya miaka miwili, adhabu yao inaweza badilika kutoka kifungo na kulipa faini, hivyoLionel Messi bado ana nafasi ya kuendelea na maisha yake ya uraiani kama kawaida kama ataamua kulipa faini.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system