“BASATA linawakumbusha wamiliki wote wa kumbi za burudani kwamba ni marufuku kukusanya watoto katika kumbi zao kupitia kile kinachoitwa ‘Disko Toto’ ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza,” limeandika kwenye taarifa yake.
“Uzoefu unaonesha kwamba, nyakati za sikukuu kama hizi za Eid El Fitr wamiliki na mameneja hawa wa kumbi wamekuwa wakijisahau na kumezwa na faida katika biashara zao kiasi cha kuandaa madisko ya watoto hali ambayo imekuwa ikisababisha maafa makubwa ambayo yangeweza kuepukwa kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu,” limesisitiza.
“BASATA mamlaka inayotoa vibali vya kumbi za sherehe na burudani linasisistiza kwamba halitafumbia macho ukumbi wowote utakaokiuka maelekezo haya sambamba na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu wa binadamu hasa yale yanayoonesha maungo ya ndani. Hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayekiuka maagizo haya. BASATA linawatakia wasanii na wadau wote wa Sanaa sherehe njema ya Eid El Fitr yenye furaha tele.
0 comments:
Post a Comment