Kocha Pep Guardiola amethibitisha kuwa sababu yake kumuacha nje kiungo huyo ni kunenepa.
Nasri, 29, aliachwa nje hata baada ya wachezaji wote wa akiba kutumika katika mechi dhidi ya Borussia Dortmund nchini China.
Hapo jana mlinzi Gael Clichy alitambua sababu ya kukosekana kwa baadhi ya wachezaji katika kambi ya mazoezi kuwa ni kunenepa.
Meneja huyo mpya wa Manchester City Pep Guardiola amewapiga marufuku wachezaji waliozidi uzito, kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza.
Pep amesema uzito ni jambo muhimu na kuwa wachezaji lazima waepuke baadhi ya vyakula na vinywaji.
0 comments:
Post a Comment