Comments


Mwana FA kushoot video yake mpya

Mwana FA
Mwana FA anatarajia kwenda tena nchini Afrika Kusini kufanya video ya wimbo wake ujao.Hiyo itakuwa video ya pili yake mwenyewe kuifanyia nje ya nchi baada ya ile iliyopita ya wimbo wake ‘Asanteni kwa Kuja.’
Akieleza sababu ya kurudi tena SA kufanya video yake, FA ameiambia Bongo5, “Kitu cha kwanza ni ile professionalism yao, ni kama watu wako very serious na kazi yao kiasi kwamba hawakupi pressure, mlichokubaliana ndio kinakwenda hivyo hivyo.”
“Cha pili hata kama ni kufanya muziki ambao utaconquer Tanzania na Afrika Mashariki kwasababu ndio soko ambalo mimi binafsi nalitolea macho, lakini bado unataka kuwa na kitu ambacho unakionesha kwamba ‘huu ni muziki wa nyumbani kwetu nimeufanya lakini naweza kumuonesha mtu yeyote Afrika na mtu yeyote duniani kwamba hii ndio video nimefanya,” ameongeza.
“Haimaanishi kwamba unataka kufanya video kwaajili ya Watanzania ufanye fanye tu kwasababu unajua viwango vyetu vilipo yaani unashindana na miguu yako mwenyewe, sio sahihi. Tunaangalia dunia inavyokwenda, kasi yake na viwango vimeshapandishwa.”
FA anaamini kuwa kwa miaka yote 14 ambayo amefanya muziki video yake ya mwisho ndio bora zaidi na hicho ndicho kitu kilichomfanya aamini katika kusafiri kwenda kufanya video Afrika Kusini.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system