Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa
ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Julai 26, 2016
anatarajia kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja
ikiwa ni maandalizi ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha
ratiba ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mkwasa
amesema lengo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016 ni kuwaweka
sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi wiki ya
mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria
unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu.
Taifa Stars
ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika
(AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu nyingine katika kundi
hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu baada ya kukusanya
pointi 10, Nigeria ina pointi mbili.
Taifa Stars mpaka sasa ina
pointi moja wakati Chad ikijiitoa katikati ya mashindano na kukatisha
ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.
0 comments:
Post a Comment