Mshindi wa tuzo ya goli bora la dunia kwa mwaka 2015 Wendell Lira ambaye ni raia waBrazil ametangaza kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 27, umri ambao kwa kawaida ilitakiwa awe anaendelea kucheza soka ila kutokana na kuandamwa na majeruhi ameamua kutangaza kustaafu soka na kujikita zaidi katika biashara za game.
Wendell Lira alishinda tuzo ya goli bora la dunia 2015 na kupewa tuzo hiyo January 2016 katika utowaji wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or, baada ya kufunga goli kwa style ya kipekee ya acrobatic katika mchezo dhidi ya Atlético-GO, baada ya kushinda tuzo hiyo Wendell alijiunga na Club Vila Nova ya kwao Brazil lakini alishindwa kufunga goli lolote katika mechi 9 alizocheza.
Video ya goli bora la dunia 2015 na alipotangazwa mshindi wa tuzo ya Puskas
0 comments:
Post a Comment