Comments


MWAKYEMBE: HATUSAJILI VIKUNDI HEWA

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema kuwa wakati wa uchaguzi mkuu kumekuwa na utitiri wa vikundi  ambavyo  havionekani kazi zake  na mwisho wa siku vinaomba msamaha wa kodi.

Akizungumza leo na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam, Mwakyembe  amesema kutokana na utitiri wa vikundi hivyo aliagiza Wakala wa Usajili ,Ufilisi na Udhamini (RITA),  kusitisha usajili wa vikundi hivyo na kufanya uchambuzi ni vikundi  ambavyo viko hai na vina vigezo kwa mujibu wa sheria.

Amesema kufanya usajili wa vikundi ambavyo kimsingi hafifanyi kazi iliyokusudiwa mwisho wa siku kuna uwezekano wa kusajili vikundi ambavyo ni hatarishi kwa taifa.

Aidha amesema kuwa kutokana na uchambuzi ambao umefanywa na kubainika kuwepo kwa vikundi 180 ambavyo vinatakiwa kufutwa kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya bodi za udhamini.

Mwakyembe baada uchambuzi huo ameitaka RITA kuendelea na kazi usajili bodi za wadhamini kwa kufuata taratibu zote na kuwa na taarifa zao.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa (RITA), Emmy Hudson amesekuwa katika uchambuzi huo kuna changamoto ambazo zilijitokeza ikiwa baadhi bodi za wadhamini kubadili ofisi pamoja na kubadili majina bila kufuata sharia.

Bi Emmy

Ameongeza kuwa bodi za wadhamini wengine wanamiliki mali bila kufuata sheria kwa mujibu sheria za RITA.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system