EURO 2016 NUSU FAINALI
Jumatano Julai 6
(Stade de Lyon)
Portugal v Wales
Alhamisi Julai 7
(Stade Velodrome, Marseille)
Germany v France
Leo huko Stade de Lyon Mjini Lyon Nchini France, Nusu Fainali ya kwanza ya EURO 2016, Mashindano ya Mataifa ya Ulaya, itachezwa kati ya Portugal na Wales.
Mechi hii inavumishwa sana kuwa ni pambano kati ya Cristiano Ronaldo dhidi ya Gareth Bale, Wachezaji Wawili wanaocheza Klabu moja, Real Madrid ya Spain.
Lakini wenyewe wamesisitiza pambano hilo si vita kati yao bali ni mtanange wa Nchi mbili.
Pambano hili lina mvuto wa kihistoria kwa Portugal kuweka historia ya kuwa Nchi ya kwanza kutinga Nusu Fainali 4 tangu Mwaka 2000.
Lakini hilo safari hii limekuja huku Portugal wakiwa hawajashinda hata Mechi moja ndani ya Dakika 90 kwa kutoka Sare Mechi zao zote za Kundi lao, kushinda 1-0 kwa Bao la Dakika ya 117 katika Dakika za Nyongeza 30 walipoitoa Croatia katika Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na katika Robo Fainali kuibwaga Poland kwa Penati baada ya Sare ya 1-1.
Nao Wales wametinga Nusu Fainali kwa mara ya kwanza na bila kutegemewa.
Kwenye Robo Fainali, Wales walitoka nyuma na kuibwaga Timu ngumu ya Belgium Bao 3-1.
Hata hivyo, Wales wanaingia kwenye Mechi hii wakiwa na dosari kwa kumkosa Kiungo wao mahiri Aaron Ramsey ambae yuko Kifungoni baada ya kupokea Kadi za Njano mbili.
Mwingine wa Wales ambae ataikosa Mechi kwa kuwa Kifungoni ni Ben Davies wakati Portugal watamkosa William Carvalho kwa tatizo hilohilo.
Mshindi wa mechi hii atakutana aidha na Ufaransa au Ujerumani katika dimba la Stade de France Jumapili
Kesho Alhamisi ipo Nusu Fainali ya Pili kati ya Wenyeji France na Mabingwa wa Dunia Germany.
Home / MICHEZO
/ NANI NI NANI KATI YA RONALDO VS GARETH BALE KUHAKIKISHA TIMU YAKE INAKWENDA FAINALI/.??/
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment