DK Kigwangala asema serikali haipo tiari kuona mapenzi ya jinsia moja
Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla ameendelea kusisitiza kuhusu vitendo hivyo na kueleza kuwa serikali haipo tayari kuona vitendo hivyo vinafanyika kwa wananchi wake lakini pia kuzitangazia mwisho wake taasisi ambazo zinafanya jitihada kutetea watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Dk. Kigwangalla ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo aliposti video ambayo ikimwonyesha akikemea vitendo hivyo na kusema kuwa serikali itazifutia usajili mara moja taasisi zote ambazo zitabainika kupokea pesa kutoka mataifa ya nje ili kutetea mashoga
Ishu ya watu ambao wanashiriki mapenzi ya jinsia moja imekuwa kubwa kiasi kwamba viongozi mbalimbali wamekuwa wakizungumza katika maeneo mbalimbali ambayo wanapata nafasi ya kuzungumza na kukemea vitendo hivyo.
0 comments:
Post a Comment