Comments


UTAFITI UNAONYESHA KUWA UNENE UNAUA MAPEMA

Utafiti wa kimataifa umegundua kuwa kunenepa
kunahusiana moja kwa moja na visa vya watu
kufa mapema, huku wanaume wakiwa katika
uwezekano mara tatu wa kufariki zaidi ya
wanawake.
Kwa kutumia data kutoka takriban watu milioni 4
kutoka mabara manne, Utafiti huo uliochapishwa
katika jarida la Lancet unaashiria kwamba watu
wanene wanakufa kwa kiasi cha miaka mitatu
mapema tofauti na watu walio na unene wa
kawaida.
Watu walio na unene wa kupindukia wanapoteza
miaka kumi ya maisha yao ambayo wangeweza
kuishi.
Wanasayansi wanasema kwamba kuwa na uzito
mkubwa wa mwili kunaongeza hatari ya kuugua
maradhi ya moyo na ya mapafu, kiharusi na
saratani.
Utafiti huo mpya unatofautiana na matokeo ya
utafiti wa awali yaliyoashiria kwamba kuwa
mnene kuna manufaa ya kuishi zaidi.
Badala yake watafiti wanasema moja kati ya vifo
vitano vya mapema Marekani na moja kati ya
vifo 7 vya mapema Ulaya, vinatokana na
kunenepa kupindukia.

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system