MSEMAJI WA CHADEMA AZUSHIWA KIFO
Msemaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, Boniface Makene amekanusha uvumi unaonezwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Kilimanjaro, Philimon Ndesamburo amefariki dunia usiku huu.
Makene amewataka Watanzania kuupuuza kwani huenda walioutengeneza wana malengo yao binafsi.
“Nimefuatilia na kupata uhakika kutoka mfumo wa chama hadi mkoani Kilimanjaro na kubaini kuwa habari hizo ni uongo mkubwa nawaomba watu na vyombo vya habari kuzipuuza,” amesema Makene.
0 comments:
Post a Comment