Comments


WAKAMATWA KWA KOSA LA KUIBA UMEME

WATU wanane wamekamatwa jijini Arusha jana baada ya kukutwa wakiiba umeme na kulisababishia hasara Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco).

Akizungumza jijini Arusha jana wakati wa operesheni ya kukamata wanaohujumu miundombinu ya shirika hilo, Mdhibiti Mapato wa Tanesco mkoa wa Arusha, Mhandisi Hassan Juma Lumuli, alisema wizi wa umeme una madhara makubwa na ndiyo maana hivi sasa wanaendesha operesheni mbalimbali za kuwabaini wahusika na kuwachukulia hatua za kisheria.

Alisema wezi hao ambao hakuwa tayari kuwataja majina yao kwa sasa, walikuwa wakichezea mita ili wasomaji mita wa Tanesco washindwe kusoma kiasi sahihi wanachodaiwa na pia kujiunganishia kinyemela kwa kupitisha nyaya chini ya ardhi.

Aidha, alisema mbali na kusababisha hasara kutokana na wizi huo, pia madhara ya kujiunganishia umeme kiholela ni mengi ikiwamo vifo na upootevu wa mali baada ya nyumba kuungua.

“Lakini tunachosikitika ni kuona kuwa baadhi ya viongozi wa kidini na wa mitaa wakiwa sehemu ya tatizo badala ya kuwa mfano mzuri kwa jamii katika kufuata sheria na kuheshimu miundombinu ya umeme ,” alisema

Akizungumzia suala hilo, Afisa Usalama wa Tanesco mkoa wa Arusha, Kembe Sabini, alisema kazi ya kukamata wezi wa umeme ni endelevu na hivyo wengine wenye tabia hiyo waache mara moja kwa sababu gharama za umeme ni za chini na kwamba, wavunjao sheria ni lazima watanaswa tu

Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system