Comments


HALMASHAURI YA WILAYA YA TEMEKE YAPEWA SIKU MOJA KUMALIZA TATIZO LA AJIRA ZA MIKATABA

NDI1Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya  Chamazi jijini Dar es salaam baada ya kuwasili shuleni hapo kukbidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya Shule za Dar es salaam  Julai 28, 2016.Wengine pichani kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam, Theresia Mmbando, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda na Mkuu wa wilaya ya Temeke  Felix Lyaviva. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NDI2Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na wananchi wa Temeke baada ya kuwasili kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi kukabidhiwa madawati na fedha shilingi milioni 100  kwa ajili ya Shule za Dar es salam  Julai 28, 2016. Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda. (Picha na Oisi ya Waziri Mkuu)
ndi4Baadhi ya wanafunzi na mmoja wa wananchi waliohudhuria hafla ya kukabidhi madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa Waziri Mkuu kwenye shule ya Msingi yaChamazi jijini Dar es salaam Julai 28, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
ndi5Waziri Mlkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Waziri wa Mambo ya Nje na  Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Balozi, Augustine Mahiga (katikati) na Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora Nchini katika hafla ya kakabidhi madawati na fedha  shilingi milioni 100 kwa shule za Dar es salaam  iliyofanyika kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016.(Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
ndi6Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Chamazi  jijini Dar es salaam baada ya kupokea madawati na fedha shilingi milioni 100 kwa ajili ya mkoa wa Dar es salaam Julai 28, 2016.Madawati ayo yalitolewa na Wizara Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki ikishirikiana na Ubalozi wa Kuwait nchini pamoja na Jumuiya ya Mabohora nchini. (Picha na Ofisi  ya Waziri Mkuu)​
ndi7Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru , Murtaza Adamjee wa Jumuiya ya Mabohora nchini baada ya kukabidhiwa madawati 105 kwenye Shule ya Msingi ya Chamazi jijini Dar es salam Julai 28, 2016. Kushoto ni Balozi wa Kuwait nchini, Jaseem Al Najem na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Dkt. Susan Kolimba. (Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Halmashauri ya wilaya ya Temeke kuondoa wafanyakazi wa mkataba kwa anjia ya kuwapa ajira ya kudumu kwa wenye sifa na kuwaondoa wasiokuwa na sifa ifikapo  Julai 30 mwaka huu.
Amesema kitendo cha kutowaajiri na kuwatumikisha kwa mikataba kwa muda mrefu kinasababisha wakose stahiki zao jambo ambalo si halikubaliki.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Julai 28, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo na kusisitiza kwamba ni lazima sula hilo lishughulikiwe haraka kwa sababu hayo ndio matundu watumishi hewa.
“Mnawatumikisha watu kama vibarua kwa muda mrefu, hapa kuna wengine wanafanya kazi kwa mikataba kwa miaka mitano hadi sita hii haikubaliki kwani mnawakosesha stahili zao pale mnapowaachisha kazi,” amesema.
Awali Kaimu Ofisa Utumishi wa Manispaa hiyo Zaitun Hassan alisema wamekuwa wakitoa ajira za mikataba kwa sababu wamekosa watu wenye sifa za kuweza kuajiriwa husan madereva.
“Kwa mara ya mwisho umetangaza lini nafasi za ajira? Katika mkoa wa Dar es Salaam kweli wanaweza kukosekana madereva wenye sifa za kuajiriwa? Alihoji Waziri Mkuu.
Zaitun alisema kuwa madereva wengi wanaojitokeza pindi wanapotangaza ajira wanashindwa kufikia vigezo ikiwemo kuwa na cheti cha VETA na badala yake wanakuwa na cheti cha kidato cha nne tu.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema kuwa kuna wafanyakazi wengine katika Idara ya Uhasibu na Ujenzi ambao nao wameajiriwa kwa mkataba hivyo amemtaka Ofisa Utumishi kuomba kibali cha kuajiri kwa Katibu Mkuu Utumishi.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kufanya tathmini ya maeneo yote ya shule kwenye mkoa wake na watakaobainika kuingia katika maeneo hayo waondolewe haraka.
Amesema baada ya kukamilisha utengenezaji wa madawati kinachofuatia sasa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambapo amezitaka halmashauri kuweka mipango  ya kujenga majengo ya madarasa ya ghorofa ili waweze kuwa na madarasa mengi katika eneo dogo.
Awali Waziri Mkuu alipokea msaada wa madawati 705 katika hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Chamazi wilayani Temeke ambapo kati yake Ubalozi wa Kuwait nchini Tanzania umetoa madawati 600 na Jumuia ya Mabohora imetoa madawati 105.
Pia Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dk. Agustino Mahiga alimkabidhi Waziri Mkuu hundi ya sh. milioni 85 fedha zilizochangwa na watumishi wa wizara hiyo kwa ajili ya kuchangia utengenezaji wa madawati.
Dk. Mahija alisema watumishi hao walichanga sh. milioni 100 kwa ajili ya utengenezaji wa madawati ambapo sh. milioni 15 wamekabidhi kwa mkuu wa wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe ambaye alikuwa mtumishi wa wizara hiyo ili naye akatengeneze madawati kwa shule za wilayani kwake.
Kwa upande wake Balozi wa Kuwait nchini Jaseem Al Najem amesema Serikali ya Kuwait itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika shughuli zote za maendeleo hususan katika sekta za elimu na afya.
Share on Google Plus

About Unknown

0 comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments System

Disqus Shortname

Comments system